MAHAKAMA Yaamuru Rais Hersi Aachie Ngazi Yanga
MAHAKAMA Yaamuru Rais Hersi Aachie Ngazi Yanga
MAHAKAMA Yaamuru Rais Hersi Aachie Ngazi Yanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Klabu ya Yanga ukiongozwa na Rais wake Eng. Hersi Said kuachia ngazi kwa sababu Katiba halali ya Yanga ya mwaka 1968 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2011 haitambui uwepo wao.
Uamuzi huo wa Mahakama umekuja baada Kundi la Wanachama wa Yanga wakiongozwa na Juma Magoma na Geofrey Mwaipopo kushinda kesi waliyoifunga Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwezi Agosti mwaka jana wakipinga katiba ya mwaka 2010 ambayo iliwaweka Madarakani Bodi ya Wadhamini ya Yanga na Uongozi mzima chini ya Rais Eng. Hersi Said.
Wanachama hao katika madai yao waliieleza Mahakama kuwa, wanaitambua katiba ya mwaka 1968 ambayo ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2011 na siyo vinginevyo.
Mahakama baada ya kusikiliza pande zote amewapa ushindi Wanachama hao kufuatia kujiridhisha kwamba katiba ya Yanga SC ya mwaka 2010 haitambuliki kisheria na haipo kwenye rekodi za RITA na katiba pekee inayotambulika ni ya mwaka 1968 ambayo ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2011.
Sehemu ya hukumu ya Mahakama imeeleza kwamba;
Bodi ya Wadhamini ya Yanga SC ambayo ipo madarakani kwa sasa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 haina uwezo wa kutawala na kuendesha mambo ya Yanga SC.
Matumizi na miamala yote iliyofanywa na Viongozi wa Yanga SC chini ya Bodi ya Wadhamini ya katiba ya mwaka 2010 ni batili.
Bodi ya Wadhamini ya Yanga SC kwa mujibu wa katiba ya 1968 iliyofanyiwa mabadiliko 2011 inatakiwa kuitisha mkutano wa Wanachama wa Yanga kwaajili ya kuchagua Wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo.
Aidha, Wanachama walioshinda kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Yanga, wameutaka uongozi wa sasa wa klabu hiyo chini ya Rais Eng. Hersi Said kuachia Madaraka, huku wakitakiwa kuwasilisha Mapato na Matumizi kwa kipindi chote walichotawala kinyume na Sheria.
Rais Eng. Hersi Said akishindwa kutoa Taarifa ya Mapato na Matumizi kama alivyoamurishwa atashtakiwa kwa Mujibu wa Sheria.