RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 7 za Kazi Wilaya ya Momba July 20-2024

Filed in Ajira, Uncategorized by on 20/07/2024

NAFASI 7 za Kazi Wilaya ya Momba July 20-2024

NAFASI 7 za Kazi Wilaya ya Momba July 20-2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Momba 20-07-2024.

NAFASI 7 za Kazi Wilaya ya Momba July 20-2024

NAFASI 7 za Kazi Wilaya ya Momba July 20-2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Momba 20-07-2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba kuomba nafasi za
kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 ya tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 5)

MAJUKUMU YA KAZI.

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye rejista;
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi;
  • Kusambaza majalada kwa watendaji;
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada au mahali pegine yanapohifadhiwa;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mwajiri au Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au kidato cha sita (Form VI).
Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada (NTA) Level 6 katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali wenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS C.

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 2)

MAJUKUMU YA KAZI.

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya Kijiji;
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi
    katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza
    uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika Kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji;
  • Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogondogo za Kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Kidato cha Nne (Form IV) Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/ cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi
    miaka 45;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha
    kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri
    wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha
    nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi
    wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.
    CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 Julai, 2024.

Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja nanvyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Momba,
S.L.P 273,
MOMBA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (anuani hii inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.)

Maombi yatakayowasilishwa nje utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags: ,

Comments are closed.