MWONGOZO wa Utumiaji Mfumo wa Udahili Vyuo vya Ualimu TCMS
MWONGOZO wa Utumiaji Mfumo wa Udahili Vyuo vya Ualimu TCMS
MWONGOZO wa Utumiaji Mfumo wa Udahili Vyuo vya Ualimu TCMS, Teacher Colleges Management System(TCMS) tudent`s Porta, Mfumo wa Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu (TCMS),Jinsi ya Kutuma Maombi Mafunzo ya Ualimu 2024/2025 MOEST TCMS.
Mwongozo huu unalenga kuwapa watumiaji maelezo kamili kuhusu jinsi ya kutumia Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu (TCMS) kwa ufanisi.
Imeundwa kwaajili ya watumiaji wote wa mfumo, wakiwemo wasimamizi wa vyuo, wafanyakazi wa udahili, wanafunzi Pamoja na Wafanyakazi makao makuu ya wizara.
Lengo kuu la mwongozo huu ni kuongoza mtumiaji hatua kwa hatua katika kila kipengele cha mfumo, kuanzia mwanafunzi anapoomba chuo, usajili na kuingia hadi usimamizi wa wanafunzi, masomo, na taarifa.
Mwongozo huu unaelezea kwa kina kazi
zote muhimu za mfumo, unatoa maelekezo ya wazi na mafupi, na unajumuisha picha za skrini na michoro ili kuifanya iwe rahisi kuelewa namana ya kutumia mfumo huu.
Malengo Mahususi ya Mwongozo
Malengo makuu ya mwongozo huu, kuboresha mchakato wa udahili na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vyuo vya ualimu.
Tunatumai mwongozo huu utakuwa
rasilimali muhimu kwa watumiaji wote wa Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa
Vyuo vya Ualimu.
Tunawahimiza watumiaji kusoma mwongozo huu kwa makini na
kufuata maelekezo kwa uangalifu ili kuhakikisha matumizi bora ya mfumo.
Ikiwa watumiaji watakumbana na matatizo yoyote au maswali, wanaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi wa mfumo kwa usaidizi.
Kwa kutumia mwongozo huu, watumiaji wataweza:
- Kuelewa vyema madhumuni na utendaji wa Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu.
- Kuelewa namna ya kutuma maombi ya kujiunga na vyuo vya ualimu kwa wanafunzi na waombajii
- Kujifunza jinsi ya kujisajili na kuingia kwenye mfumo.
- Kudhibiti mchakato wa udahili wa wanafunzi, kuanzia kupokea maombi hadi kutoa barua za uandikishaji.
- Kuendesha masuala ya wanafunzi, kama vile usajili wa kozi, malipo ya ada, na
ufuatiliaji wa mahudhurio. - Kudhibiti mipango ya masomo, kozi, na ratiba za masomo.
- Kuunda na kutoa ripoti mbalimbali kuhusu wanafunzi, masomo, na shughuli za chuo.
- Kutatua matatizo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati wa kutumia mfumo.
- Watumiaji wa Mwongozo
Mwongozo huu utatumika na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na
Watumishi katika vyuo vya ualimu kupitia moduli mbalimbali za mfumo. - Pia mfumo utatumika na wanafunzi watakaokuwa wanataka kujiunga na vyuo vya
Ualimu katika kozi mbalimbali kwa ajili ya kufanya udahili, usajili na kuona maendelkeo ya kitaaluma.
KUJISAJILI
jinsi ya kujisajili kwenye mfumo wa udahili, Kiunganishi (Link)
Tembelea Kiunga cha Mfumo kwa kutumia kivinjari (browser) chochote kisha andika kiunganishi (link) cha mfumo waUdahili na Usimamizi vyuo vya Chuo cha Ualimu https://tcm.moe.go.tz Baada ya kufungua hiyoo linki, Ukurasa wa nyumbani utafunguka.
MWONGOZO wa Utumiaji Mfumo wa Udahili Vyuo vya Ualimu TCMS
Kwenye ukurasa wa nyumbani kuna maelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Application status, Pia kuna
paneli ya viunganishi vya Mfumo (System links) ambavyo ni Login, Kutengeneza akaunti ya mwombaji (Create Account) Mwongozo wa Udahili (Admission GuideBook) Pomoja na Sehemu ya Kuona Mwongozo wa kutumia mfumo (System Usermanual).
Kwenye ukurasa wa mbele, nenda kwenye paneli ya viunga vya Mfumo
Kutengeneza akaunti
- Chagua cha Create Account ili kuweza kutengeneza akaunti ya kukuwezesha kuomba chuo
- Kwenye dirisha ibukizi, Hatua ya 1 ni Usajili wa taarifa za kitaluma kutoka NECTA
- Andika nambari ya kidato cha nne mfano S3610/0052.
- Chagua mwaka uliomaliza kidato cha nne kutoka kushuka chini (drop down)
- Bofya Kitufe cha Register, ukishasajili kwa mafanikio Mfumo utakupeleka hatua
ya pili ya usajili.
Kuingiza/Kujaza taarifa Binafsi
- Hatua ya pili ya Usajili ni kujaza taarifa binafisi, Jina, jinsi na namba ya mtihani
wa kidato cha nne vitavutwa moja kwa moja kutoka NECTA. - Itaonyesha (Majina ya mwombaji, Jinsia, nambari ya Kidato cha 4, ongeza nambari
ya simu, chagua tarehe ya Kuzaliwa, chagua uraia) - Ongeza taarifa za Makazi (Anwani ya Mahali, Mkoa na wilaya)
- Ingiza Vitambulisho vya Kuingia (Anwani ya Barua pepe, Nywila na Thibitisha
Nywila) Kama inavyoonekana hapa juu kwenye picha - Bonyeza kitufe cha Usajili, Register
Kuhakiki barua pepe
M. Baada ya Kubonyeza kitufe cha kujisajili yaani Register Utatumiwa kiunganishi (link) kwa ajili ya kuhakiki barua pepe yako ili kukuwezesha kuingia kwenye akaunti yako
kwenye mfumo huu wa udahili.
Tembelea barua pepe yako, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini, kisha bonyeza kwenye kiunganishi (link) kilichotumwa kwenye barua pepe ili kuweza kuhakiki akaunti yako ambapo itakupeleka kwenye ukurasa wa kuingia kwenye mfumo.
LOGIN
Jinsi ya kuingia kwenye mfumo (login)
Hatua za kufuata ili kuweza kuingia kwenye mfumo
- Tembelea link ya mfumo https://tcm.moe.go.tz:8081/
- Nenda upande wa wa kulia sehemu imeandikwa System Links
- Bonyenya kwenye Login.
Ukurasa wa kufikia (Landing Page)
Ukisaha ingia kwenye mfumo utakutana na Dashibodi kama inavyoonyeshwa hapo chini.
Baada ya kufungua kikamilifu, Bonyeza Apply for Admission.
JINSI YA KUFANYA UDAHILI.
Kuchagua Tangazo
Hatua inayofuata ni kuchagua aina ya tangazo kwa ajili kuomba kozi, Hapa unaweza kuta matangazo Zaidi Zaidi ya moja, lakini unachagua tangazo linaloendana na vigezo vyako, kwa maana kuna kozi zingine zinahitaji matokeo ya kidato cha sita, mengine
kidato cha nne.
Ili kuweza kuendelea mbele bonyeza Apply
Ukurasa wa kuchagua Tangazo la Udahili linaonekana, Chagua Tangazo ili uweze
kuomba kozi.
Hakiki taarifa za kielimu (Kidato cha Nne)
Baada ya kubonyeza Apply Dashibodi inayoonyesha matokeo ya kidato cha nne inakuja na kukagua kama matokeo ndo ya kwako/mwanafunzi, ili kuweza kuendelea mbele, Bonyeza batani ya chini kulia imeandikwa Apply
Taarifa za Kidato cha Sita
Baada ya kubonyeza Apply, dashibodi ya kuingiza namba ya kidato cha sita inaonekana, kama ulisoma kidato cha sita ingiza namba na mwaka wa kumaliza baada ya kuingiza Bonyeza Apply, kama hauna au hukusoma kidato cha sita Bonyeza skip ili mfumo ukupeleke hatua inayofuata.
Taarifa za Ualimu Daraja La IIIA.
Baada ya kubonyeza Next, Ukurasa wa kuweka Taarifa za Walimu daraja la Tatu A (Teacher Grade A Certificate Examination (GATCE).
Kwenye huu ukurasa watajaza
waliosoma ualimu daraja la IIIA, wanaotaka kujiendeleza kusoma Diploma. Wale ambao hawana GATCE Watabonyeza kitufe cha Skip.
Taarifa za Ualimu Daraja La IIIA.
Baada ya kubonyeza Next, Ukurasa wa kuweka Taarifa za Walimu daraja la Tatu A (Teacher Grade A Certificate Examination (GATCE).
Kwenye huu ukurasa watajaza
waliosoma ualimu daraja la IIIA, wanaotaka kujiendeleza kusoma Diploma. Wale ambao hawana GATCE Watabonyeza kitufe cha Skip.
Chagua programu na Kozi (Course selection)
Baada ya kubonyeza Apply Ukurasa wa kuchagua program na kozi linaonekana kwaajili ya kuchagua kozi.
Baada ya kufanya machagua matatu bofya kitufe cha Next. Ili kuweza kwenda ukurasa unaofuata ambao ni ukurasa wa kuchagua taarifa za mahitaji maalumu.
TAARIFA ZA MAHITAJI MAALUMU
Asiye na Mahitaji Maalumu
Taarifa za Mahitaji maalumu.Kama mwombaji hana mahitaji maalumu chagua No.Baada ya kuchagua No bonyeza kitufe cha Next.
Mwenye mahitaji maalumu.
Kama mwombaji atakuwa na mahitaji maalumu atachagua Yes, kisha kwenye dropdown atachagua aina ya Mahitaji malumu kwenye dropdown, kisha atajaza maelezo mafupi kwenye kiboksi cha maelezo. Kisha Bonyeza Next.
TAARIFA ZA JUMLA ULIZOJAZA HAPO JUU
Baada ya kubonyeza Next, Dashibodi ya kuangalia taarifa na kozi uliyochagua inatokea kama inavyoonekana hapo chini. Baada ya hapo bonyeza Submit Application.
Taarifa Binafsi
Taarifa za Course ulizochagua
Taarifa za Kidato cha Nne.
Taarifa za Kidato cha Sita.
Taarifa za Mahitaji Maalumu
MREJESHO WA MAOMBI
Baada ya kubonyeza Submit Application Maombi ya chuo yanakamilika na unapata ujumbe hapo chini.
MSAADA
Ili kuweza kupata usaidizi wa mambo mbalimbali kuhusu udali bonyeza hiyo linki hapopembeni ili uweze kuchati na maafisa udahili kwa msaada Zaidi.
Kwa kumalizia, mwongozo huu umetupa mwanga juu ya hatua muhimu za kutumia mfumo wa udahili katika vyuo vya ualimu Tanzania.
Kwanza kabisa, Utangulizi umetoa
muhtasari wa mfumo huu na umuhimu wake katika kuhakikisha upatikanaji wa walimu wenye sifa.
Hatua za Kujisajili kwenye Mfumo na Kuingia kwenye Mfumo zimefafanuliwa kwa kina ili kuhakikisha watumiaji wanaweza kuanza mchakato wa
udahili bila matatizo yoyote.
Aidha, mwongozo umeeleza kwa undani jinsi ya Kufanya Udahili kwa Kuchagua Kozi ya Kusoma Chuoni, hatua ambayo ni msingi wa mafanikio ya mtumiaji katika safari yake ya Elimu.
Kwa kuzingatia vipengele hivi, mtumiaji anaweza kutumia mfumo huu
kwa ufanisi na kuhakikisha anachagua kozi sahihi katika chuo kinachomfaa.
Pamoja na kueleza hatua hizi, ni muhimu kutambua kwamba kuboresha uzoefu wa watumiaji katika mfumo wa udahili ni mchakato endelevu.
Hivyo basi, tunapendekeza
yafuatayo:
- Mafunzo na Msaada: Kutoa mafunzo ya mara kwa mara na msaada kwa watumiaji wapya ili kuhakikisha wanafahamu vizuri jinsi ya kutumia mfumo.
- Marekebisho ya Mfumo: Kufanya maboresho ya mara kwa mara kwenye mfumo
ili kuboresha ufanisi na urahisi wa matumizi. - Ushirikiano: Kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuleta maboresho endelevu.
Kwa kufuata mwongozo huu, tunaamini watumiaji wataweza kufanya udahili kwa ufanisi na kwa urahisi, hivyo kusaidia kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania.
Mwisho kabisa, ni jukumu letu sote kuhakikisha mfumo huu unatumika ipasavyo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kwa msaada wowote wa kutumia mfumo au mchakato wa udahili piga 0737 962 965 au tuma barua pepe kwa [email protected]
Tags: MWONGOZO wa Utumiaji Mfumo wa Udahili Vyuo vya Ualimu TCMS