WATUHUMIWA Mauaji ya Mtoto Asimwe Wafikishwa tena Mahakamani
WATUHUMIWA Mauaji ya Mtoto Asimwe Wafikishwa tena Mahakamani
WATUHUMIWA Mauaji ya Mtoto Asimwe Wafikishwa tena Mahakamani, Leo July 26,2024 imeitwa tena kwa mara ya tatu kesi ya Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu Mkoani Kagera May 30 mwaka huu 2024 na June 17, 2024 mwili wake ukakutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake.
Watuhumiwa hao tisa wamefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwaajili ya kutajwa tena shtaka lao ambapo Wakili wa Serikali Erick Mabagala amesema kuaa bado wanaendelea kushughulikia utaratibu wa kusajili shauri hilo katika Mahakama Kuu ambayo ndo ina Mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia na uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika, shauri hilo limeitwa tena mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson ambaye amesema kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamerudishwa rumande mpaka August 9,2024 ambapo kesi yao itatajwa tena huku wakisubiri kukamilishwa kwa jalada lao.
Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora (49) ambaye ni Padri, Novat Venant (24) ambaye ni Baba wa Mtoto Asimwe, Nurdin Ahmada, Ramadhan Selestine, Rwenyagira Alphonce,Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist huku baadhi yao wakitoa machozi wakiwa Mahakamani.
Miongoni mwa Watuhumiwa hao, Mshitakiwa namba moja ambaye ni Padri Elpidius Rwegoshora tayari ameweka Wakili wa kumtetea aitwaye Mathias Rweyemamu.
Tags: WATUHUMIWA Mauaji ya Mtoto Asimwe Wafikishwa tena Mahakamani