RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

Filed in Habari by on 27/07/2024

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

Na Mariam Kagenda_Kagera

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA kutoka jimbo la Bukoba Vijijini, Bi Conchesta Rwamulaza amewakutanisha zaidi ya vijana mia nne (800) kutoka Kata zote za Halmashauri hiyo ili wapatiwe Elimu ya Usalama Barabarani na namna ya kuepuka kufanya Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambapo Elimu hiyo imetolewa na Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Wilaya ya Bukoba.

Mheshimiwa Rwamulaza amesema kuwa kutokana na changamoto ya kuongezeka Kwa Vitendo vya Ukatili hususani kwa Watoto ikiwemo pia ajali za Barabarani ambazo wakati mwingine zinasababishwa na vijana hao ambao wengi wao ni boda boda ameamua kuwakutanisha kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao ili wapatiwe Elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama BarabaraniMbali na utolewaji wa Elimu ,pia Mbunge huyo ametoa vifaa vya Michezo kwa timu 11 za mpira za vijana kutoka Halmashauri ya Bukoba ikiwemo mipira 11 na jezi za michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa.

Kwa upande wao Maafisa wa Jeshi la Polisi waliotoa Elimu kwa vijana hao akiwemo Mkuu wa dawati la jinsi Wilaya ya Bukoba, Bi Betrida Mbinga na Coplo wa usalama Barabarani Mohamed Sadick wamemshukuru Mbunge huyo Kwa kuwa na maono makubwa ya kuwakutanisha vijana hao ili wapatiwe Elimu ambayo itawasaidia kujiepusha na Ukatili pamoja na masuala ya ajali zinazoweza kuepukika.

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

VIJANA Jimbo la Bukoba Vijijini Wanufaika na Elimu ya Usalama Barabarani

Baadhi ya vijana hao wamemshukuru Mbunge huyo kwa kukutanisha kundi kubwa la vijana bila kujali itikadi za vyama vyao.

Vijana hao wameweza kumpatia Mbunge huyo zawadi ya vitu mbalimbali kama shukrani kutoka kwa vikundi vya vijana wanaofanya shughuli za ujasiliamali kupitia vikundi kwa ufadhili wa Mbunge huyo aliowapatia mtaji kwa miaka miwili iliyopita na sasa wameanza kunufaika.

Tags:

Comments are closed.