RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Wilaya ya Kongwa July 31-2024

Filed in Ajira by on 31/07/2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Kongwa July 31-2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Kongwa July 31-2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Kongwa July 31-2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Kongwa July 31-2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kufuatia kupokea kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora anawatangazia watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kutuma maombi ya kujaza nafasi ya kazi kama ifuatavyo;

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI MBILI (2)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwa safari za kazi;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
  • Kutunza na kujaza daftari la safari “log book” kwa safari zote;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha Nne (IV). Awe na leseni ya daraja la “C” au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria Mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali, yaani TGS B

MASHARTI YA JUMLA:

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye Umri kati ya Miaka 18 hadi 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea Ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, Namba za Simu na Anuani ya barua pepe (E-mail addres) pamoja
    na majina ya Wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • ‟Provisional/Testimonials/Statement of results‟‟ na hati za matokeo za Kidato cha Nne
    na Sita) Form IV na VI results Slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatishe Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na Vyeti vya Taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni Vyeti vya Kidato cha Nne na Vyeti vya kuhitimu
    mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishiwa na Mamlaka (TCU NACTE na NECTA)
  • Uwasilishaji wa Taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Agosti, 2024.

Muhimu: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na Vyeti ya Elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa,
S.L.P 57,
KONGWA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia Anuani ifuatayo; htts//:portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretatieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ’Recruitment Portal).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags:

Comments are closed.