RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 20 za Kazi Manispaa ya Singida July 31-2024

Filed in Ajira by on 01/08/2024

NAFASI 20 za Kazi Manispaa ya Singida July 31-2024

NAFASI 20 za Kazi Manispaa ya Singida July 31-2024

NAFASI 20 za Kazi Manispaa ya Singida July 31-2024

NAFASI 20 za Kazi Manispaa ya Singida July 31-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.

Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

MTENDAJI WA MTAA DARAJA III – NAFASI 10

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
  • Mratibu na msimamizi wa upangaji wa mipango shirikishi ya maendeleo ya Mtaa;
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
  • Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na sheria nyingine zinazotumika
    katika Mtaa;
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na
    umaskini katika mtaa;
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa na;
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA MWOMBAJI
Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV/VI waliohitimu stashahada (NTA Level 6) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Usimamizi wa Fedha (Finance Management), Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS B.

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelekezwa na Msimamizi wako

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha Nne (Form Four) na leseni Daraja C au E ya uendeshaji magari ambaye amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au
chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS B

MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMIIDARALA LA II – NAFASI 5

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kusaidia na kupanga mipango na Miradi ya Maendeleo katika eneo lake.
  • Kusaidia uwezeshaji na upatikanaji wa mafunzo kuhusu masuala ya maendeleo katika eneo lake.
  • Kusaidia kutoa elimu kuhusu kazi za kujitegemea katika eneo lake.
  • Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
  • Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya Jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji
    na kwa msimamizi wake wa kazi.
  • Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo
  • Kutambua na kuwezesha Kaya maskini kuinua uchumi wao kupitia fursa na rasilimali
    zinazowazunguka.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Waombaji wenye cheti cha mtihani wa kidato cha nne (IV) au sita (VI ) wenye
Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), Sayansi ya Jamii (Sociology), masomo ya Maendeleo
(Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development au fani nyingine zinazofanana na Maendeleo ya Jamii.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS B

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II NAFASI 3

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuorodhesha barua zinazoingia kwenye regista (incoming correspondence register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers).
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye shabaka/ kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatailia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya kidato cha nne IV) au sita (VI), aliyehitimu stashahada (NTA level 6) katika fani ya Utunzji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
mwenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
    kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
    wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya
    kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
    (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 13 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –

Mkurugenzi wa Manispaa
Halma 236,
SINGIDA

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayo wasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

 

Tags:

Comments are closed.