NACTVET Matokeo ya Udahili wa Vyuo vya Afya Awamu ya Kwanza
NACTVET Matokeo ya Udahili wa Vyuo vya Afya Awamu ya Kwanza
NACTVET Matokeo ya Udahili wa Vyuo vya Afya Awamu ya Kwanza,MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI KWA KOZI ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautangazia umma matokeo ya uchaguzi wa awamu ya kwanza kwa walioomba kujiunga na programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Jumla ya waombaji 24,629 waliwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS).
Waombaji 23,503 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda. Waombaji 21,661 walikuwa na sifa kwenye programu
walizoomba na waombaji 1,842 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba.
Jumla ya waombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo wanawake 8,821 (53%) na wanaume 7,825 (47%).
Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba wanashauriwa kuomba kujiunga katika programu na
vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya pili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.
Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwa kubonyeza CAS Selection 2024 kwaajili ya kupata taarifa zaidi.
Aidha, Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya pili limefunguliwa rasmi leo tarehe 11/07/2024 na litakuwa wazi hadi tarehe 10/08/2024, matokeo ya uchaguzi yatatolewa tarehe 16/08/2024.
Tags: NACTVET Matokeo ya Udahili wa Vyuo vya Afya Awamu ya Kwanza