RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 27 za Afisa Utalii MDAs na LGAs August 2024

Filed in Ajira by on 04/08/2024

NAFASI 27 za Afisa Utalii MDAs na LGAs August 2024

NAFASI 27 za Afisa Utalii MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 26 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.

NAFASI 27 za Afisa Utalii MDAs na LGAs August 2024

NAFASI 27 za Afisa Utalii MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 26 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.

✅AFISA UTALII DARAJA LA II (NAFASI 27)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na wadau
    wote;
  • Kutoa Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii;
  • Kukusanya na kuweka takwimu zawatalii na safari za kitalii;
  • Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi;
  • Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii;
  • Kutoa ushauri wa kitalaam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii;
  • Kuandaa kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii;
  • Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli;
  • Kukagua hoteli, loji na migahawa;
  • Kujibu na kufuatilia malalamiko yanayoletwa na watalii;
  • Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia na kutoka wageni;
  • Kutunza Kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii;
  • Kukusanya taarifa ya kila mwezi ya takwimu za watalii walioingia nchini na mapato yaliyopatikana;
  • Kufanya tafiti ndogo (Survey) kwenye Hifadhi za Taifa na maendeleo tengefu ili kupata
    idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii;
  • Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini;
  • Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii;
  • Kutayarisha ripoti ya mwezi, robo mwaka na za mwaka mzima;
  • Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya survey;
  • Kuitisha mikutano ya Tourism Facilitation Committee;
  • Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kutuatilia utekelezaji wa maazimio;
  • Kupitia miongozo inayohusu “Tourism Facilitation Committee;
  • Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii;
  • Kutayarisha na kuhakiki vivutio vya utalii nchini;
  • Kuitisha mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii;
  • Kushiriki katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii;
  • Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimbali za mazingira katika shughuli zihusuzo utalii
    na mazingira; na
  • Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii
au Hoteli kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
    cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama
    ifuatavyo;.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
    Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
    Cheti cha kuzaliwa
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags: , , ,

Comments are closed.