INEC Walioitwa kwenye Usaili Mkalama District Council
Kwa kuzingatia Kanuni 12 (b) ya Kanuni za uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura za mwaka 2024 pamoja na Tangazo la nafasi za kazi za muda za Watendaji wa vituo vya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura la tarehe 15 Aprili, 2024 linalohusu nafasi ya Mwandishi Msaidizi na Mwendeshaji wa vifaa vya Bayometriki (BVR).
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Iramba Mashariki anapenda kuwatangazia Waombaji wa Kazi za Mwandishi Msaidizi na Mwendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki (BVR) waliokidhi vigezo kufika kwenye usaili.
MAELEKEZO YA JUMLA KWA WASAILIWA WOTE
Usaili wa mahojiano utafanyika kuanzia tarehe 04 Septemba, 2024 kuanzia Saa 2:00 asubuhi kwa mchanganuo ufuatao;
- Wasailiwa kutoka Kata ya Mwangeza, Nkinto na Mwanga watafanya usaili tarehe 04/09/2024 katika Shule ya Sekondari Mwangeza.
- Wasailiwa kutoka Kata ya Ibaga, Mpambala, Gumanga na Matongo watafanya usaili tarehe 05/09/2024 katika Shule ya Sekondari Ibaga.
- Wasailiwa kutoka Kata ya Iguguno, Tumuli, Kikhonda na Kinyangiri wafanya usaili tarehe 06/09/2024 katika Shule ya Sekondari Iguguno.
- Wasailiwa kutoka Kata ya Nduguti, Msingi, Nkalakala, Miganga, Ilunda, na Kinampundu watafanya usaili tarehe 07/09/2024 katika Shule ya Sekondari Mkalama One.
Waombaji wote wanatakiwa kufika na vyeti halisi (original certificates).
Aidha atakayekuja na “Transcript” au “result slip” pekee bila vyeti halisi hataruhusiwa kufanya usaili.
Ofisi ya Afisa Mwandikishaji Jimbo la Iramba Mashariki haitahusika na gharama zozote za wasailiwa katika kipindi chote cha usaili (Usafiri, Chakula na Malazi)
Ofisi hii inawajulisha kuwa hakuna gharama yeyote inayohusiana na malipo ili kuitwa kwenye usahili, hivyo inawataadharisha kujiadhari na utapeli unaoweza kutokea na kupewa maelekezo mengineyo ambayo hayahusiani na usaili.
Orodha ya Majina ya wasailiwa imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;
DONWLOAD PDF KUITWA KWENYE USAILI INEC – MKALAMA DC