RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva

Filed in Makala by on 14/07/2024

AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva

AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva, Jinsi ya kuangalia leseni ya Udereva, Leseni ya udereva 2023, Madaraja ya leseni ya udereva tanzaniaz Mfano wa leseni ya udereva, Leseni ya udereva vip, Namba Ya Leseni ya Udereva.

AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva

AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva, Jinsi ya kuangalia leseni ya Udereva, Leseni ya udereva 2023, Madaraja ya leseni ya udereva tanzaniaz Mfano wa leseni ya udereva, Leseni ya udereva vip, Namba Ya Leseni ya Udereva.

A-Pikipiki zenye Ukubwa wa zaidi ya 125CC au uzito wa 230Kg ikiwa na kigari pembeni au isiyokuwa na kigari.

A1 – Pikipiki zenye Ukubwa chini ya 125CC au uzito 230kg na isiyokuwa na kigari pembeni.

A2 – Kuendesha pikipiki za magurudumu matatu au manne.

A3 – Mitambo ya kukatia majani au pikipiki zisizozidi 50CC.

B – Magari aina zote (Binafsi) ISIPOKUWA Magari ya Biashara, Magari Makubwa ya Mizigo na Pikipiki.

C – Magari ya kubeba abiria kuanzia 30 na kuendelea.

C1 – Magari ya kubeba abiria 15 hadi 29.

C2 – Magari ya kubeba abiria 4 hadi 14.

C3 – Magari ya kati ya abiria 4 hadi 14.

D-Magari aina zote ISIPOKUWA Magari ya Abiria, Magari Makubwa ya Mizigo na Pikipiki.

E-Magari aina zote ISIPOKUWA Magari ya Abiria na Pikipiki.

F – Mitambo kama Graders, Folklift n.k

G – Mitambo ya Mashambani na Migodini kama Tractors n.k

H – Leseni ya kujifunzia kuendesha Gari.

NB: Unapokuwa na Daraja D huna haja ya kuwa na daraja B kwa kuwa daraja D hujumuisha magari yaliyo katika daraja B ila ukiwa na daraja B huwezi endesha daraja D.

Pia ukiwa na daraja A si kigezo cha kuendesha madaraja yote ya A, utaendesha Madaraja yote ya A isipokuwa A2 ambayo ni Pikipiki za Magurudumu Matatu/Manne.

Kuomba Leseni ya Udereva kwa mara ya kwanza ni lazima uwe umehudhuria mafunzo katika Chuo chochote kinachofahamika na kupewa cheti.

Pia uwe na umri zaidi ya miaka 18 kwaajili ya Gari na umri wa miaka 16 na kuendelea kwaajili ya pikipiki.

Uwe na Leseni ya kujifunzia/ya muda ya Udereva.

Uwe umelipa Ada ya kufanyiwa majaribio – GRR, Bei za leseni ya udereva, Aina za leseni za udereva, Jinsi ya kuangalia leseni yako mtandaoni, Madaraja ya leseni ya udereva, Madaraja ya leseni pdf, Jinsi ya kupata leseni ya udereva online.

Uwe na Cheti cha kupimwa macho, uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya Polisi wa Usalama Barabarani kwaajili ya kufanyiwa majaribio.

Uende kwenye Ofisi ya Polisi wa Usalama Barabarani ukiwa na Gari kwaajili ya kufanyia majaribio.

Baada ya mwombaji kufanyiwa majaribio anaweza kuruhusiwa kuendesha pikipiki na magari madogo.

  • Mwombaji ataenda kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
  • lazima awe na cheti cha umahiri
  • mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka  16 kwa pikipiki

KUBADILI ILI KUPATA DARAJA ”C”

  • Mwombaji ataenda katika ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
  • Awe na cheti cha umahiri
  • Mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16 kwa pikipiki
  • Cheti cha Gari la Kubeba Abiria (PCV) kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji au VETA
  • Mwombaji anatakiwa kubainisha aina ya gari analokusudia kuendesha
  • Mwombaji atapewa daraja la leseni kulingana na mafanikio yake.
Viwango vya leseni za udereva ni:
Ada za leseni Shilingi 40,000/= itakayolipwa kila baada ya miaka 3
Ada ya jaribio la kuendesha Shilingi 3,000/=
Ada za leseni ya muda Shilingi 10,000/= itakayolipwa kila baada ya miezi 3

Tags: , , , , , , , , , , ,

Comments (2)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Gharama za kupata leseni daraja A ni bei gani

  2. Gharama za kupata leseni daraja B ni bei gani?