AJIRA Mpya 37616 Kada za Ualimu, Afya, Uhasibu na Ugavi 2024
AJIRA Mpya 37616 Kada za Ualimu, Afya, Uhasibu na Ugavi 2024
AJIRA Mpya 37616 Kada za Ualimu, Afya, Uhasibu na Ugavi 2024, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, amesema kuwa Serikali imepanga kutangaza Ajira mpya 37,616.
Amesema Ajira za Kada ya Ualimu, Afya, uhasibu, ugavi na kada nyinginezo tayari zinaendelea kutangazwa, lengo likiwa ni kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi nchini.
Alisema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Kitete, Laela, Kamsamba na Kavifuti vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipouteliwa kushika wadhifa huo.
Akizungumzia nafasi za ajira za ualimu ambazo tayari zimeshatangazwa na Sekretarieti ya Ajira kwenye ngazi ya mikoa kulingana na mahitaji ya mkoa husika, Sangu alisema utaratibu wa kuwapata walimu kwa mwaka huu umeanza kuwa wa tofauti ukilinganisha na miaka ya nyuma.
AJIRA Mpya 37616 Kada za Ualimu, Afya, Uhasibu na Ugavi 2024
Alisema kuwa usaili huo umeanza kufanyika kwa kada ya ualimu kwa sababu nafasi za ajira za ualimu ni chache ukilinganisha na idadi ya walimu wa shule ya msingi na sekondari waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini, ambapo zaidi ya walimu 100,000 wapo mtaani hawana ajira.
Sangu alisema serikali imekuja na uamuzi huo ili kuchagiza dhana ya ushindani kwa lengo la kuhakikisha kila mwenye sifa stahiki anapata ajira katika mazingira aliyopo pasipo kulazimika kusafiri kwenda Dodoma au Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya usaili.
Sangu alitoa wito kwa vijana waliohitimu vyuo mbalimbali nchini kuchangamkia nafasi hizo, huku akiwataka wajiandae kwaajili ya usaili.
Tags: Afya, AJIRA Mpya 37616 Kada za Ualimu, Uhasibu na Ugavi 2024