RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya

Filed in Michezo, Usajili by on 10/07/2024

AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya

AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya

AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya

AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amethibitisha kuwa bado yupo sana.

Kauli ya Aziz Ki inamaliza sintofahamu ya Mfungaji Bora huyo wa Ligi Kuu msimu uliopita wa 2023/2024 kuhusu hatma yake ndani ya Young Africans ambapo alikuwa akihusishwa na Vilabu vya nje.

Aziz Ki ametua nchini Alfajiri ya leo akitokea mapumzikoni nchini kwao Burkina Faso na baada ya hapo akasaini Mkataba Mpya wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia Wananchi hadi 2026.

Aziz Ki ambaye alijiunga na Young Africans SC msimu wa 2022-2023 akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, ameitumikia Yanga kwa misimu miwili, hivyo kuongeza miaka miwili mingine inamaanisha atakuwa Mwananchi mwa miaka minne.

AZIZ Ki Asaini Mkataba MpyaNdani ya misimu hiyo miwili ya kwanza, Aziz Ki amekuwa na mchango mkubwa wa upatikanaji wa mafanikio ikiwemo Makombe ya Ligi Kuu ya NBC na FA ambayo yote Yanga imeyabeba misimu mawili mfululizo yeye akiwemo Ngao ya Jamii mara moja.

Aziz Ki pia anakumbukwa kwa namna ambavyo msimu wa 2022/2023 ambao Yanga ilicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, goli lake pekee katika mchezo wa Marudiano dhidi ya Club Africain ndilo liliipeleka Yanga hatua ya Makundi ya Michuano hiyo na kuwa safari ya kwenda Fainali ikachochewa hapo.

Msimu uliopita ambao ilibaki kidogo Yanga ifuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Aziz Ki alifunga goli ambalo lilikataliwa dhidi ya Mamelodi Sundowns ugenini.

Goli hilo lilizua mjadala mkubwa katika soka la Afrika na nje ya Bara hili huku baadaye Rais wa CAF, Patrice Motsepe akikiri wazi kwamba lilikuwa goli halali ingawa maamuzi ya VAR ililikataa kwa madai mpira haukuvuka mstari.

Aziz Ki katika misimu miwili ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na jezi ya Young Africans, amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 30 na hat trick tatu, AZIZ Ki Asaini Mkataba Mpya.

Msimu wa 2022/2023 alifunga magoli 9 ikiwemo hat trick moja dhidi ya Kagera Sugar, huku msimu wa 2023-2024 akifunga magoli 21 na hat trick mbili dhidi ya Azam na Tanzania Prisons kisha akaibuka kuwa Mfungaji Bora wa Ligi hiyo.

Aziz Ki ameonekana kuvutiwa na project ya Young Africans kutaka kubeba Ubingwa wa Afrika na usajili mzuri uliofanyika ndani ya Klabu hiyo kitu kilichompa matumaini makubwa ya kufikia malengo yake ndiyo maana ameamua kuongeza mkataba mpya.

AZIZ Ki Asaini Mkataba MpyaIkumbukwe kwamba, nyota huyo raia wa Burkina Faso, alikuwa akiwindwa vikali na timu kubwa barani Afrika ikiwemo Mamelodi Sundowns, CR Belouzidad, Wydad Casablanca, Al Ahly, Raja Casablanca na nyinginezo, lakini akaamua kubaki Young Africans.

Aziz Ki hakubaki tu kirahisi, bali ushawishi mkubwa alionao mwekezaji wa klabu hiyo, Gharib Said Mohamed (GSM) na Rais wa Young Africans, Injinia Hersi Said umesababisha yote hayo kutokea.

Injinia Hersi ndiye aliyemshawishi mara ya kwanza kusaini Young Africans kipindi anatoka ASEC Mimosas kwani nyota huyo pia alikuwa akiwindwa na timu kubwa za ndani ya Afrika na Ulaya, lakini ushawishi huo unaochagizwa na GSM na project iliyopo ikamvutia Kiungo huyo.

Kuongeza mkataba kwa Aziz Ki ni sehemu ya kuendelea kuboresha kikosi Cha Young Africans kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 ambapo hadi sasa Klabu hiyo imefanikiwa kuwabakiza Wachezaji Saba waliokuwepo msimu uliopita Kwa kuwaongezea mikataba.

Wachezaji hao ni Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa Pamoja na Aziz Ki.

Mbali na hao, pia Young Africans imefanikiwa kusajili wachezaji wapya watano mpaka sasa ambao ni Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Khumeiny Aboubakar na Aziz
Andambwile.

Tags:

Comments are closed.