RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


BENCHIKHA na Simba wamalizana

Filed in Michezo, Usajili by on 28/04/2024

BENCHIKHA na Simba wamalizana

BENCHIKHA na Simba wamalizana

BENCHIKHA na Simba wamalizana

BENCHIKHA na Simba wamalizana, Klabu ya Simba muda wowote kuanzia sasa itatangaza kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mualgeria, Abdelhak Benchikha ikiwa ni siku moja tangu atwae Kombe la Muungano lililohitimishwa jana visiwani Zanzibar.

Simba ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0, lililofungwa na kiungo Babacar Sarr katika dakika ya 77 na kuwapa Simba Ubingwa wa sita wa michuano hiyo baada ya kulitwaa kuanzia mwaka 1993, 1994, 1995, 2001, 2002 na 2024.

Klabu hiyo inaachana na Benchikha baada ya kudumu kwa siku 156 tangu alipotambulishwa Novemba 24, mwaka jana akichukua nafasi ya Robertinho Oliveira ‘Oliveira’.

Inaelezwa kuwa maombi ya kuondoka katika timu hiyo aliyatuma Jumamosi April 20 usiku.

Sababu alizoambatanisha kwenye ombi lake ni kushidwa kutimiza malengo ya timu kama alivyowaahidi hasa upande wa CAF Champions league lakini pia kubwa zaidi ni kuuguliwa na mmoja wa watu wake wa Karibu hivyo anahitaji kuwa naye Karibu zaidi.

Kiongozi aliyetumiwa taarifa hiyo alijaribu kuona ni jinsi gani wana maliza tatizo la mgonjwa wake huyo huku pia akimuomba aendelee na programu ya kuandaa mazoezi ya timu kama kawaida kitu ambacho Benchikha alikubali.

Ni kweli tumeshidwa kufanya vyema katika mashindano zaidi ya matatu chini yake ila bado uongozi ulitamani kuendelea naye kwa msimu ujao kwa manufaa ya timu ila sasa safari hii Benchikha anaamini ni wakati wake na mgonjwa yule kuwa naye karibu zaidi kwao na sio Tanzania tena ili kumuuguza.

Changamoto ambazo wengi wanazisema kuhusu Usajili ni kweli zipo.

Lakini Simba uwezo wa kusajili mchezaji kwa Dollar 3,000 bado na hakuna timu yenye uwezo huo kwa Tanzania hii hata Afrika mashariki na Bora awe Mchezaji mmoja ila zaidi ya mmoja ni ngumu kitu ambacho kocha aliambiwa na hakuwa nayari nacho pia.

Tags:

Comments are closed.