CRDB Mdhamini Mpya Kombe la Shirikisho la TFF
CRDB Mdhamini Mpya Kombe la Shirikisho la TFF
CRDB Mdhamini Mpya Kombe la Shirikisho la TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Benki ya CRDB, wamesaini mkataba wa udhamini wa Kombe la Shirikisho (CRDB Bank Federation Cup) wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa miaka mitatu na nusu.
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakisaini mkataba wa udhamini wa Kombe la TFF leo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa miaka mitatu na nusu.
Makubaliano hayo yanaifanya Benki ya CRDB kuwa Mdhamini wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya wilaya.
Udhamini huu wenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.79 utakuwa wa miaka mitatu na nusu kuanzia hatua ya 16 Bora Msimu huu wa 2023/2024.
Katika zoezi la utiaji saini, viongozi mbali mbali kutoka TFF na Benki ya CRDB walihudhuria akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Ndugu. AbdulMajid Nsekela, Rais wa TFF, Bw. Wallece Karia, watendaji mbalimbali kutoka TFF, Wafanyakazi wa CRDB Bank pamoja na waandishi wa habari.
Kuanzia sasa michuano hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakuwa ikitambulika kama CRDB Bank Federation Cup.