RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


DKT Nchimbi Aagiza Ulipaji Fidia Waliopisha Mradi wa Upanuzi wa Barabara Bukoba Mjini

Filed in Habari by on 12/08/2024

DKT Nchimbi Aagiza Ulipaji Fidia Waliopisha Mradi wa Upanuzi wa Barabara Bukoba Mjini

DKT Nchimbi Aagiza Ulipaji Fidia Waliopisha Mradi wa Upanuzi wa Barabara Bukoba Mjini

DKT Nchimbi Aagiza Ulipaji Fidia Waliopisha Mradi wa Upanuzi wa Barabara Bukoba Mjini

DKT Nchimbi Aagiza Ulipaji Fidia Waliopisha Mradi wa Upanuzi wa Barabara Bukoba Mjini,Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuelekeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kuiwezesha Wizara ya Ujenzi kiasi cha Shilingi Bilioni 1.8 kwaajili ya malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa upanuzi wa njia nne wa barabara ya Bukoba Mjini kuanzia Rwamishenye Round About hadi Stendi Mpya ya Bukoba Mjini (km 1.2) ambao utekelezaji wake unaendelea.

Dkt. Nchimbi ametoa maelekezo hayo Mkoani Kagera wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Bukoba Mjini ambapo pamoja na mambo mengine amesikiliza na kutatua kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi.

“Nitumie nafasi hii kumtumia salamu Waziri wa Fedha huko huko alipo kwa uzito wake, Dkt. Mwigulu hawezi kushindwa kutafuta Bilioni 1.8 kwa muda mfupi, Kwahivyo naielekeza Wizara ya Fedha kutafuta hizi fedha haraka sana kwa ajili ya fidia za wananchi wa Bukoba Mjini”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.

Awali, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inaendelea na upanuzi wa barabara njia nne kuanzia Rwamishenye Round About hadi Stendi Mpya ya Bukoba Mjini ambapo ujenzi huo ukikamilika itaendelea na Awamu ya Pili kuanzia Rwamishenye hadi Stendi Mpya ya Kyakailabwa na Awamu ya Tatu kuanzia Stendi ya Mpya ya Bukoba Mjini hadi Bandari ya Bukoba (Customs).

Aidha, Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mingi ya kimkakati katika Sekta mbalimbali na hata ile ambayo ipo katika mpango wa kuanza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Ndege cha Omukajunguti Mkoani Kagera.

Kwa upande, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Stephen Byabato ameeleza kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 16 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara inayoendelea kutekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika jimbo la Bukoba Mjini.

Tags:

Comments are closed.