RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga

Filed in Michezo by on 29/04/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga

ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga

ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga

ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga, Rais wa Yanga Hersi Said amesema kuwa amekabidhiwa Young Africans kama Rais akiwa na miaka 37, Sio rahisi kijana mdogo kama yeye kukabidhiwa timu kongwe yenye miaka 89 na mafanikio makubwa.

Akifanya mahojiano na kituo Cha Radio cha Bongo FM, Hersi ameongeza kuwa baada ya kukabidhiwa walipambana kuhakikisha wale waliokuwa wana fikra kuwa vijana hawawezi, wanabadili fikra hizo.

Hersi ameongeza kuwa kwa sasa hakuna Klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Young Africans SC kwenye ubora. Ndio maana timu nyingi zikicheza na nao zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu Klabu hiyo.

Amesema kuwa Malengo yake makubwa ni kuhakikisha Klabu hiyo inakuwa moja ya Klabu Bora.

ENG Hersi aeleza njia ya Mafanikio ya Yanga“Matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora AFRIKA, ili tuweze kushiriki kombe la Dunia la vilabu. Mwaka jana tumefika Fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki kombe hilo”

“Usajili ni sanaa, ni lazima ujue kwanini unafanya huo usajili. Kwa kifupi huwezi kubaki na Wachezaji wako wazuri kwa muda wote, hivyo inabidi utengeneze mazingira mazuri ya kuvutia Wachezaji wengine wazuri. Hivyo nilichukua maamuzi ya kusimamia mchakato wa usajili”

“Unapokuwa kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira. Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzuoea mazingira, amechoka nk. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia” Alisema Eng. Hersi

Hersi pia aligusia suala ya Wachezaji kutoka Vilabu vikubwa kutamani kuichezea Young Africans.

“Ukweli ni kwamba kuna wachezaji kadhaa kutoka Klabu kubwa wanataka kujiunga na Klabu yetu. Ni kwa sababu wanaona uimara wa Uongozi, wadhamini na uwepo wa GSM.

Pia mashabiki wetu ni sehemu ya usajili huwezi kuwakwepa mashabiki, wanaweza kukuonyesha mchezaji mzuri kwahiyo kuna wakati unapaswa kusikiliza sauti za mashabiki” Eng. Hersi

Hersi pia amesema kuwa hajawahi kujuta kuitumikia Young Africans.

“Sijawahi kujuta kuwepo Yanga, ni taasisi ambayo ipo kwenye moyo wangu muda wote, challenges ambazo nakutana nazo ni challenges ambazo zinahitaji busara na nimekuwa nikipata ushauri kutoka kwa wazee wangu, viongozi wangu akiwemo Ghalib”

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.