RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


FISTON Mayele Kutua Simba SC

Filed in Michezo, Usajili by on 06/04/2024

FISTON Mayele Kutua Simba SC

FISTON Mayele Kutua Simba SC

FISTON Mayele Kutua Simba SC

FISTON Mayele Kutua Simba SC, Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Pyramids FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, Fiston Mayele amesema kuwa lolote linawezekana kuhusiana na uamuzi wa kujiunga na Klabu ya Simba SC msimu ujao wa 2024/2025.

Mayele alijiunga na Pyramids mwaka jana baada ya kuichezea Yanga kwa mafanikio ambapo msimu uliopita aliisaidia kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).

Mshambuliaji huyo amekuwa akihusishwa na Simba Kuelekea msimu ujao ili kuimarisha safu ya Ushambuliaji ambayo kwa sasa ni tatizo linalowasumbua zaidi Wekundu hao wa Msimbazi.

Akizungumza baada ya kutembelea kambi ya Simba nchini Misri ambayo jana usiku iliwakabili wenyeji, Al Ahly katika mechi ya marudiano ya hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), Mayele mwenye umri wa miaka 29 alisema kuwa mpira ni kazi yake na muda utakapofika kila kitu kitawekwa wazi.

“Kwa kweli tumuombe Mungu, tumalize msimu, na Inshaa Allah chochote kinawezekana,” alisema kwa ufupi Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans.

FISTON Mayele Kutua Simba SCMkongomani huyo alisema amefanikiwa kuitazama Simba katika Mashindano ya kimataifa na kuona ina tatizo katika safu ya Ushambuliaji ambayo ingekuwa vyema, ilikuwa na uwezo wa kuamua matokeo kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam.

Alisema katika mashindano makubwa safu ya Ushambuliaji ndio huamua Matokeo kwa sababu michezo hiyo ni ya kutumia kila nafasi zinazopatikana.

“Mimi kama mchezaji niliangalia mechi ya kwanza Tanzania, wenzangu walipambana, Simba walitengeneza nafasi, lakini hawakuzitumia vizuri. Siongei hayo kwa sababu mimi ni Mshambuliaji bali kwa kuwa nimeangalia mchezo wa kimataifa,” Mayele alisema.

Kutokana na safu yake ya Ushambuliaji kutofanya vyema, Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, alilazimika kutumia siku tano baada ya mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali kuwanoa mastraika kwaajili ya mchezo wa jana usiku.

Benchikha aliandaa dozi maalumu kwa lengo la kutumia vyema kila nafasi itakayopatikana na hatimaye Simba kufikia malengo yake.

Katika kuboresha safu ya washambuliaji ya Simba, wakati wa dirisha dogo iliwasajili Fred Michael na Pa Omar Jobe, ambao bado hawajaonyesha makali yanayotakiwa na kikosi hicho.

Simba pia inaamini bado inaweza kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo linashikiliwa na watani zao, Yanga huku pia Azam FC ikiwa kwenye vita ya kumaliza msimu wa 2023/2024 katika nafasi mbili za juu.

FISTON Mayele Kutua Simba SC

Tags:

Comments are closed.