FORM SIX Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024 Awamu ya Pili 2024
FORM SIX Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024 Awamu ya Pili 2024
FORM SIX Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024 Awamu ya Pili 2024, Majina ya Walioitwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024,PDF JKT Form Six Selection 2024, How to View JKT Selection for Form Six in 2024.
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2024 AWAMU YA PILI
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesikia kilio cha wazazi na walezi wa wahitimu wa kidato cha sita ambao waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kwa mujibu wa sheria, lakini hawajaripoti baada kuwaruhusu kwenda kwenye kambi zilizo karibu na makazi yao.
Hivi karibuni Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Rajabu Mabele alitoa wito kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa lazima mwaka 2024.
Vijana hao walitakiwa kuripoti katika kambi walizopangiwa wakiwa na vifaa walivyoainishiwa, kuanzia Juni 01, 2024 hadi Juni 7, 2024.
Leo Juni 22, 2024, Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena aliwatangazia vijana wote walioitwa katika mafunzo hayo ya lazima lakini hawajaripoti kambini hadi sasa, kuripoti mara moja katika kambi za karibu.
Amesema uamuzi wa kuwataka kuripoti katika makambi yaliyo karibu badala ya yale waliochaguliwa awali, unatokana na jeshi hilo kupokea maombi kutoka kwa wazazi na walezi ya kuomba kubadilishiwa kambi.
Brigedia Jenerali Mabena amesema kwa kawaida vijana wanaenda kusoma katika maeneo tofauti nchini, hivyo kutokana na utaratibu wa kuwapangia kambi zilizopo karibu na shule walizosoma wengine wanajikuta wakilazimika kugharamia nauli kubwa kwenda kuripoti.
“Lakini unaweza kukuta kijana anakwenda kusoma Songea (Ruvuma) lakini yeye anaishi Musoma (Mara). Na wote tunajua hali za kiuchumi. Tumekuwa tukipata simu nyingi sana kutoka kwa wazazi na baadhi ya walezi wakiomba vijana wao kubadilishiwa kambi,” amesema.
Amesema wengi wa vijana waliopangiwa walishindwa kuripoti kwa kukosa nauli na kwa kuwa walezi na wazazi walionyesha changamoto hiyo wakati walipokuwa wakiwapigia simu, JKT imeamua kuwaruhusu kuripoti katika makambi yaliyo jirani.
“Sisi tulizingatia hili ndio maana katika tangazo hili tumewaambia kuwa vijana hawa (wasioripoti hadi sasa), waripoti katika kambi zilizopo karibu yao ,” amesema Brigedia Jenerali Mabena.
“Inawezekana kijana anaishi Arusha lakini alipangiwa kambi iliyoko Rukwa na ameshindwa kusafiri sasa ili apate fursa hii kambi iliyoko karibu na kwake inaweza kuwa Olijoro ama Makuyuni popote pale,” amesema.
Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amesema JKT imetoa nyongeza awamu ya pili ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024, kujiunga na jeshi hilo ili kufanya mafunzo hayo ya lazima.
Brigedia Jenerali Mabena amesema vijana hao wote wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia leo hii Juni 22,2024 hadi tarehe Juni 26,2024.
Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.
- Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue.
- Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne nk.
- Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo awamu ya pili na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz
JKT Selection Camps Tanzania releases Form six 2024-25 PDF
KUONA MAJINA BONYEZA HAPA
Aidha, majina hayo pia yanapatikana kupitia simu ya mkononi, kwa mtumiaji kupiga USSD CODE *152*00#, kisha atachagua No 8 (Elimu) ikifuatiwa na No 5 (JKT), ambapo mtumiaji ataingiza namba ya shule aliyosoma ikifuatiwa na majina yake matatu kisha mtumiaji ataoneshwa kambi alilopangiwa na mahali ilipo.
Huduma hii inapatakana kwa watumiaji wa mitandao yote ya simu nchini.
For more information Visit Official JKT Website http://www.jkt.go.tz/
PDF JKT Form Six Selection 2024,www.jkt.go.tz 2024,Nafasi za kujiunga na JKT 2024, Mafunzo ya jkt ni muda gani, Kambi Za JKT Tanzania, www.jkt.go.tz matangazo, Form six Jkt Selection 2024 Pdf, Waliochaguliwa Jkt 2024 Awamu ya Pili, JKT Form Six Selection (PDF List).
Tags: FORM SIX Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024 Awamu ya Pili 2024, How to View JKT Selection for Form Six in 2024, MAJINA ya Walioitwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024, PDF JKT Form Six Selection 2024
Nimechaguliw
I want to be selected please
I want to be selected to join with jkt