FURSA ya Ufadhili wa Masomo kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2024/2025
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza fursa ya Ufadhili wa Masomo ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalumu.
Maombi yanakaribishwa kwa wanachuo wanaosoma, Stashahada ya Elimu maalumua katika maeneo yafuatayo:
- Ulemavu wa Akili
- Usonji
- Uziwi
- Uziwi Kutoona na
- Ulemavu wa Uoni.
SIFA ZA KUPATA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi wenye sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania;
- Awe amepata udahili katika Chuo cha Ualimu kinachotambulika na Serikali na kinatoa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu;
NAKALA ZA KUWASILISHA
- Barua ya kuomba ufadhili ikionesha kozi unayosoma, namba ya simu na barua pepe;
- Nakala ya vyeti vya kitaaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria;
- Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria; na
- Barua kutoka kwa Mkuu wa Chuo ikionesha kuwa umedahiliwa katika Chuo husika.
MAENEO YA UFADHILI
Ufadhili utahusisha maeneo yafuatayo:
- Ada ya Mafunzo;
- Michango mingine ya Chuo (Mf. Ulinzi,ukarabati n.k);
- Vifaa vya kufundishia na
- kujifunzia;
- Nauli; na
- Bima ya Afya.
MASHARTI YA UFADHILI
Mwanachuo atakayepata ufadhili kwa ajili ya kusoma Stashahada ya Elimu Maalumu atawajibika kuzingatia masharti yafuatayo:
- Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
- Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwaajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja;
- Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila idhini ya Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
- Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na Daktari kutoka katika Kituo cha Afya au Hospitali inayotambuklika na Serikali;
- Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili, atapaswa kutoa taarifa kwa maandishi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Mkuu wa chuo alichodahiliwa na kujisajili.
MUDA WA UFADHILI
Ufadhili huu ni kwa kipindi cha miaka miwili (02) ya masomo kwa wanachuo watakaokidhi vigezo viliyobainishwa katika kipengele Na. 5.
UTARATIBU WA KUOMBA UFADHILI
Maombi yawasilishwe Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya siku 15 kuanzia Septemba 01, 2024 hadi Septemba 15, 2024.
Maombi yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, S.L.P 10 Dodoma.
Orodha ya Wanachuo watakaokuwa wamepata ufadhili huo itawekwa katika tovuti ya Wizara (www.moe.go.tz).
Tags: FURSA ya Ufadhili wa Masomo kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2024/2025