HESLB dirisha la Maombi ya Mikopo 2024/2025 lafunguliwa
HESLB dirisha la Maombi ya Mikopo 2024/2025 lafunguliwa
HESLB dirisha la Maombi ya Mikopo 2024/2025 lafunguliwa, Bodi ya mikopo kutoa Bilioni 787 kwa wanafunzi, yatoa miezi 3 Wanafunzi waombe mikopo, Msimu wa Uombaji Mikopo kwa mwaka 2024/2025 Wafunguliwa.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imefungua dirisha la kupokea maombi ya Mkopo kwa mwaka 2024/ 2025 kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali ya vyuo vikuu ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 787 kimetengwa kwa wanafunzi 224,056.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Dkt. Bill Kiwia amesema uombaji wa Mikopo umeanza June 6, 2024 hadi August 31,2024 na hakutakuwa na dirisha la pili la maombi ya mkopo huo hovyo kuwahimiza wanafunzi kuanza mara moja kuomba mkopo
“Tumetoa muda wa miezi 3 kwa wanafunzi kuomba mkopo, muda huu ndo mrefu zaidi na tunaamini unatosha kwa wanafunzi kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda na baada ya hapo hatutakuwa na muda mwingine ” amesema Dkt Bill Kiwia
Mbali na hilo pia amesema “Kama mtakavyokumbuka, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwaajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000. Idadi hi ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024. Hivyo, mwaka ujao wa masomo kutakuwa na ongezeko la jumla ya wanafunzi takribani 25,944,”
Pia Dkt. Kiwia aliwakumbusha wanahabari kuhusu miongozo mitano ya utoaji mikopo iliyozinduliwa Mei 27, 2024 na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (Mb), kuwa ni pamoja na;
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Awali (Bachelor) kwa 2024 -2025,
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada (Diploma) kwa 2024 – 2025,
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Stashahada ya Umahiri katika Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kwa 2024 – 2025 (Post Graduate Diploma in Legal Practice),
- Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Shahada za Umahiri na Uzamivu, na
- Mwongozo wa Utoaji Ruzuku za Samia kwa mwaka 2024 – 2025
“Miongozo hiyo inapatikana kwenye tovuti yetu ya Bodi ya Mikopo ya www.heslb.go.tz toka Juni 01, 2024 na nawasihi waombaji mikopo kusoma na kuielewa miongozo hiyo kabla ya kuanza kufanya maombi ya mkopo, pamoja na kuzingatia muda uliopangwa wa kujaza maombi ya mkopo wa siku tisini (90), kuanzia Juni 01 hadi Agosti 31, 2024”, amesisitiza Dkt. Kiwia.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kiwia ameelezea jinsi HESLB ilivyojipanga kutoa huduma kwa waombaji mikopo kwa kuwa na dawati maalum la kusaidia wateja wanaokwama wakati wa kujaza maombi yao au kuhitaji ufafanuzi zaidi kwa kupiga simu kwenye namba 0736 665 533 au kutuma ujumbe wa “WhatsApp’’ kwenda namba 0739 665 533.
Tags: HESLB dirisha la Maombi ya Mikopo 2024/2025 lafunguliwa
Naomba kujua kuhusu wanafunzi waliomaliza kidato Cha SITA 2024, Wanaweza kuanza taratiibu za kuomba mikopo?
Kama jibu ni hapana,Ni lini wataanza walau hatua za awali?