RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


HESLB Vipengele na Viwango vya Mikopo 2024/2025

Filed in Ajira, Habari, Makala by on 30/06/2024

HESLB Vipengele na Viwango vya
Mikopo 2024/2025

HESLB Vipengele na Viwango vya Mikopo 2024/2025, Viwango vya Mikopo vinavyotolewa Na Bodi ya Mikopo HESLB 2024/2025, Heslb vipengele na viwango vya mikopo 2024-2025,Heslb vipengele na viwango vya mikopo 2024-25,dirisha la mkopo 2024/2025,HESLB login, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma.

HESLB Vipengele na Viwango vya
Mikopo 2024/2025

HESLB Vipengele na Viwango vya Mikopo 2024/2025, Viwango vya Mikopo vinavyotolewa Na Bodi ya Mikopo HESLB 2024/2025, Heslb vipengele na viwango vya mikopo 2024-2025,Heslb vipengele na viwango vya mikopo 2024-25,dirisha la mkopo 2024/2025,HESLB login, Mwongozo wa kuomba mkopo diploma.

Vipengele vya Mkopo na Viwango vya Juu vya Fedha Waombaji watakaopangiwa mikopo watapangiwa viwango vya fedha kulingana
na uhitaji wao.

Kiasi cha jumla cha juu cha fedha kitagawanywa katika vipengele vya mkopo kwa mtiririko ufuatao:

  • Chakula na Malazi (MA)
  • Ada ya Mafunzo (TF)
  • Gharama za Vitabu na Viandikwa (BS)
  • Mahitaji Maalumu ya Kitivo (SFR)
  • Gharama za Utafiti (RES) na
  • mwisho Mafunzo kwa Vitendo (FPT).

HESLB itatoa mkopo kugharamia vipengele vyote au baadhi ya vipengele, kama ifuatavyo:-

Chakula na Malazi (MA) Kiwango cha juu cha MA kitakokotolewa kwa TZS 10,000.00 kwa siku wakati wa mafunzo chuoni kulingana na kalenda ya chuo katika mwaka husika wa masomo.

Viwango vya Ada ya Mafunzo (TU)
Kiwango cha juu cha ada ni TZS 3,100,000.00 kwa mwaka kulingana na gharama zinazolipwa katika taasisi za umma za Elimu ya Juu.

Gharama za Vitabu na Viandikwa (BS) Kiwango cha juu cha TZS 200,000.00 kwa mwaka kwa vitabu na viandikwa na
kitatolewa kwa wanafunzi wahitaji wenye sifa.

Mahitaji Maalumu ya Kitivo (SFR)
Kwa kuzingatia king’amua uwezo, mwombaji anaweza kupangiwa mkopo wa Mahitaji Maalumu ya Kitivo hadi asilimia mia moja (100%) kwa programu zenye mahitaji maalumu ya kitivo zilizoidhinishwa na TCU/NACTVET kwa kuzingatia viwango vilivyoidhinishwa kutumika katika vyuo vya umma.

Mafunzo kwa Vitendo (FPT) Bodi itatoa kiasi cha TZS 10,000.00 kwa siku hadi siku 56 kwa mwaka, kwaajili ya Mafunzo kwa Vitendo.

Mikopo kwaajili ya Mafunzo kwa Vitendo itatolewa kwa programu zinazohitaji Mafunzo kwa Vitendo kama zitakavyopendekezwa na vyuo husika vya elimu ya juu na kuidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Gharama za Utafiti (RES) HESLB inaweza kutoa hadi TZS 500,000.00 kwaajili ya kugharimia utafiti katika baadhi ya Programu za Sayansi ya Afya, Uhandisi, Kilimo na Sayansi ya Ardhi.

Programu nyingine za shahada ya kwanza zinaweza kupata mkopo kwa ajili ya utafiti kwa kiasi kisichozidi TZS 100,000.00 katika mwaka wa mwisho wa masomo.

Soma zaidi; HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025

Tags: , , , , ,

Comments are closed.