JINSI ya Kupata vyeti vya Kuzaliwa kwa walio nje ya nchi
JINSI ya Kupata vyeti vya Kuzaliwa kwa walio nje ya nchi
JINSI ya Kupata vyeti vya Kuzaliwa kwa walio nje ya nchi, Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi,Jinsi ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa njia ya mtandao.
Fahamu Utaratibu wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa, kwa Watu Walio nnje ya Nchi.
Hatua ya Kwanza:
- Tuma barua pepe ya maombi kupitia [email protected]
- Ambatanisha na kimojawapo kati ya viambatanishi vifuatavyo (Clinic card, Cheti cha ubatizo, School leaving certificates [Shule ya msingi, Sekondari]), kwa uhakika wa tarehe ya kuzaliwa mtoto, sehemu ya uzaliwa na uraia wa wazazi.
- Pakuwa fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya siku 90, lakini chini ya miaka 10), au fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya miaka 10). Jaza na zitume kwa barua pepe [email protected]
Fomu za kupakuwa zinapatikana hapa
Hatua ya Pili:
- Utapokea barua pepe kutoka RITA, iliyoambatanishwa na fomu ya Afidavit, kutoka kwa Msajili Mkuu.
- Printi na jaza fomu ya Afidavit, kisha iambatanishe na picha 3 za passport size.
- Scan fomu ya Afidavit, itume kwa barua pepe kuelekea [email protected]
Hatua ya Tatu:
- Utapokea barua pepe kutoka RITA, ikikupa ruhusa ya kulipia.
- Malipo ya kusafirisha cheti yatategemea huduma utakayoamua kutumia (DHL, EMS n.k)
Malipo:
- Cheti cha mtoto chini ya miaka 10 – $14.
- Cheti cha mtoto zaidi ya miaka 10 – $20.
- ku-clear cheque – $20.
Tanbihi:
- Utatakiwa ufanye uchunguzi ili kufahamu Malipo ya kusafirisha Cheti ni bei gani, halafu utume fedha (ya kulipia cheti), pamoja na fedha ya kukombolea mzigo(fedha).
- Tunasisitiza malipo kwa fedha taslimu.
Tags: Fomu ya cheti cha kuzaliwa., Jinsi ya kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto, Jinsi ya kupata Cheti cha kuzaliwa kilichopotea pdf, Jinsi Ya Kupata cheti Cha kuzaliwa Kwa mtu mzima, Jinsi ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa njia ya mtandao, JINSI ya Kupata vyeti vya Kuzaliwa kwa walio nje ya nchi, RITA Tanzania Cheti Cha Kuzaliwa, Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi