RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


KANISA la Kiboko ya Wachawi Lafungwa

Filed in Habari by on 27/07/2024

KANISA la Kiboko ya Wachawi Lafungwa

KANISA la Kiboko ya Wachawi Lafungwa

KANISA la Kiboko ya Wachawi Lafungwa

KANISA la Kiboko ya Wachawi Lafungwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeagiza kufungwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, Temeke – Dar es Salaam baada ya kanisa hilo kwenda kinyume cha taratibu za usajili.

Barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 imewaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dominique Kashoix Dibwe kufunga tawi la Kanisa hilo linaloendeshwa na Mchungaji huyo.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa za kufungwa kwake ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika Jamii na Mahubiri ambayo ni kinyume na maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.

Madai mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu Madhabahuni, kutoa Mahubiri Chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume cha matakwa ya kifungu cha 17 cha Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali Namba 3 ya Mwaka 2019, vyenye athari ya kusababisha kanisa hilo kufutiwa usajili wake na kuondolewa kwenye Rejista ya Jumuiya za Kiraia zilizosajiliwa.

Barua hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha imetolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa imesema, madai hayo yanakwenda kinyume cha imani ya Kikristo, Katiba na kanuni za kanisa hilo, ikiwamo kuweka kiwango cha Sh500,000 kwa waumini kupata huduma ya maombezi.

Nakala za barua hiyo zimepelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwaajili ya kuchukua hatua stahiki.

“Kutokana na hali hiyo, kwa barua hii, unajulishwa kuwa unatakiwa kufunga mara moja shughuli na huduma zote zinazotolewa katika kanisa hiyo kabla ya tarehe 28/07/2024,” imesema sehemu ya barua hiyo.

Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali imeagiza kufungwa Kanisa hilo, baadhi ya vitu kanisani hapo vimeondolewa..

Tags:

Comments are closed.