KANUNI Mpya za Ligi zilizoongezwa kwenye Toleo la 2024
KANUNI Mpya za Ligi zilizoongezwa kwenye Toleo la 2024
KANUNI Mpya za Ligi zilizoongezwa kwenye Toleo la 2024,Katika kuongeza uwajibikaji na hamasa kwa klabu wakati wa maandalizi ya michezo ya Ligi, klabu zimepewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za maandalizi ya mchezo ukiwemo mchakato wa kuuza tiketi kwa njia ya Elektroniki.
Muongozo wa uuzaji tiketi utatolewa na TFF/TPLB.
- Mamlaka ya kuandaa na kusimamia ugawaji wa vitambulisho vya msimu pamoja na mialiko ya watu maalum (VVIP) na jukwaa la watu maalum, yatakuwa chini ya TFF na TPLB.
- Kila klabu italazimika kuteua na kuitangaza angalau siku moja katika kila mwezi, ambayo itakuwa maalum kwaajili ya wanahabari kufanya mahojiano na wachezaji, maafisa wa ufundi na viongozi wa klabu kwa lengo la kuitangaza timu na Ligi kwa ujumla.
- Kutakuwa na siku maalum ya mdhamini mwenye haki ya matangazo ya runinga kutangaza matukio ya timu moja ya Ligi Kuu kuanzia maandalizi ya mwisho ya mchezo (mazoezi), chakula cha mchana, kuwasili uwanjani pamoja na baadhi ya matukio ya chumba cha kuvalia.
- Timu ya Ligi Kuu inawajibika kuutangaza kila mchezo wa nyumbani wa Ligi kwa kutumia njia mbalimbali na kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa sauti uwanjani kwaajili kutoa burudani na matangazo kwa mashabiki.
- NEW Amaan Complex Ruksa Kutumika Ligi Kuu 2024/2025
Kuhusu Makocha
- Kocha mkuu wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau Pro Diploma.
- Kocha msaidizi wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau A Diploma au inayofanana nayo.
- Kocha wa timu ya Ligi Kuu kutoka nje ya Tanzania ni lazima awe amefundisha klabu ya Ligi Kuu au timu ya Taifa katika nchi yoyote au ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kuhusu Timu kutofika Uwanjani
- Timu itakayoshindwa kufika kituoni katika michezo mitatu (3) ya Ligi bila sababu za msingi zinazokubalika na TFF/TPLB itakuwa imejiondoa kushiriki Ligi hiyo.
- Katika michezo ya mchujo, timu iliyomchezesha mchezaji aliyethibitishwa usajili wake lakini aliyebainika kubadili jina kwa nia ya kudanganya au kubainika kutumika udanganyifu mwingine wowote kufanikisha kukamilisha usajili wake au mchezaji aliyebainika usajili wake kuwa na kasoro baada ya kuthibitishwa italipa faini kati ya shilingi milioni (1,000,000/-) na shilingi milioni tano (5,000,000/-) na itakuwa imepoteza mchezo huo na hadhi ya kuendelea hatua inayofuata, timu pinzani itapewa alama tatu na mabao matatu pamoja na hadhi ya kuendelea hatua inayofuata bila kujali matokeo ya mchezo mwingine uliochezwa.
- Katika michezo ya mchujo timu itakayobainika kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa itapoteza mchezo husika, italipa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000/-) na mchezaji husika atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili (12) bila ya kujali kulalamikiwa au la, itakuwa imepoteza mchezo huo na hadhi ya kuendelea hatua inayofuata, timu pinzani itapewa alama tatu na mabao matatu pamoja na hadhi ya kuendelea hatua inayofuata bila kujali matokeo mchezo mwingine uliochezwa.
- Kutakuwa na shindano la Kombe la Muungano ambalo litahusisha timu mbili kutoka Tanzania Visiwani na mbili kutoka Tanzania Bara.
- Michezo ya Ligi inaweza kuchezwa kwenye viwanja vilivyopo Tanzania visiwani (Zanzibar) kwa mazingatio ya Kanuni 9 kuhusu Uwanja.
- Timu ya Ligi Kuu itakayoshindwa kufuata na kutekeleza masharti yote yaliyoainishwa kwenye Kanuni ya Leseni za klabu, itaadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni hizi.
Aidha ni ni marufuku kwa Kocha, Mchezaji, Kiongozi au Ofisa wa Mchezo Kushiriki Michezo ya Kubashiri (Betting).
Kocha, Mchezaji, Kiongozi au Ofisa wa Mchezo atakayekiuka, atafungiwa Maisha kujihusisha na Mpira wa Miguu.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KANUNI MPYA ZA LIGI ZILIZOTANGAZWA KWENYE TOLEO LA 2024
Tags: KANUNI Mpya za Ligi zilizoongezwa kwenye Toleo la 2024