KANUNI na Masharti ya Kufungua na Kutumia Akaunti ya M-KOBA
KANUNI na Masharti ya Kufungua na Kutumia Akaunti ya M-KOBA
KANUNI na Masharti ya Kufungua na Kutumia Akaunti ya M-KOBA
1.MKATABA NA KUTUMIKA KWAKE
1.1.Mkataba huu umeweka Kanuni na Masharti kamilifu (ambayo humu yanajulikana kama “Masharti ya Matumizi“) ambayo yatatumika katika Akaunti ya M-KOBA (kama yalivyotafsiriwa humu) itakayofunguliwa na wewe (kama itakavyotafsiriwa humu) na sisi (kama itakavyotafsiriwa humu).
1.2.Kanuni na Masharti haya na marekebisho au mabadiliko yoyote yataanza kutumika katika tarehe ya kuchapishwa kwake.
1.3.M-Pesa Limited kwa kushirikiana na TPB Bank imeanzisha mfumo mpya ili kuweka pesa, kupata mikopo na kuchangia mapato katika vikundi kama vile familia na marafiki, pamoja na vikundi/VICOBA tofauti kwa makusudi ya kutunza fedha na kupeana mikopo. Huduma hii inaitwa, M-KOBA, M-KOBA ni njia mpya ya kidijiti ya akiba ambayo inatoa usalama wa fedha za kikundi, uwazi na urahisi wa wanachama kuchangia wakiwa popote kwa kwa njia ya M-Pesa ya Vodacom.
1.3.1.M-Koba imeanzishwa ili kutatua changamoto za sasa zilizovikabili vikundi vyenye utaratibu unaohusiana na fedha kama vile ukusanyaji salama wa michango kutoka kwa wanachama, kutoa mikopo na kuchangia mapato. M-Koba ni kitu kingine muhimu cha kuifikisha Tanzania katika uchumi wa Kidijiti kwani kinaondoa ulazima wa kubeba fedha taslimu kwa ajili ya shughuli za kikundi.
1.4.Kanuni na Masharti haya yatatumika na kufuatwa na wateja wote wa M-PESA na Wasiokuwa Wateja wa M-Pesa ambao wanatumia huduma ya M-Koba (kama ilivyofafanuliwa humu). Marekebisho au mabadiliko yoyote yatakayofanywa katika Kanuni na Masharti haya yataanza kutumika katika tarehe ya kuchapishwa kwake au kama itakavyoelezwa vinginevyo katika marekebisho na mabadiliko hayo na yatatumwa katika Tovuti na au kufahamishwa kwa arafa na au mitandao ya Kijamii; kwa wasiokuwa wateja wa M-Pesa, Viongozi wa vikundi wanawajibika pia kuwafahamisha wanachama wao iwapo kutatokea marekebisho yoyote kama yalivyotajwa katika 2.1.3 hapo chini.
1.4.1.Unathibitisha kuwa umesoma na kuelewa Kanuni na Masharti ya Matumizi, na jedwali/kiambatisho chochote pamoja na Kanuni & Masharti ya Jumla ya Benki, Kanuni na Masharti ya Mteja wa M-Pesa na Kanuni na Masharti ya Mteja wa GSM ambayo yatakuwa sehemu ya Kanuni na Masharti haya.
2.UFAFANUZI2.1.Katika Kanuni na Masharti haya, maneno na maelezo yafuatayo (yatatumika pale muktadha utakavyotaka vinginevyo) yatabeba maana zifuatazo:
2.1.1.“Akaunti ya Kikundi ya M-KOBA” maana yake ni akaunti inayomilikiwa na Mteja na ambayo ilifunguliwa na kuendeshwa kulingana na Kanuni na Masharti ya Matumizi yaliyomo humu;
2.1.2.“Benki” maana yake TPB Bank PLC iliyoandikishwa nchini Tanzania kama kampuni yenye dhima yenye ukomo chini ya sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 yenye leseni kamili kama benki chini ya Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006;
2.1.3.“Masharti ya Matumizi” maana yake ni Kanuni & Masharti haya; yakijumuisha marekebisho yoyote na kiambatisho chochote, majedwali, vizibiti, faharasa au vyote vitakavyoambatishwa au kujumuishwa kwa ajili ya marejeo katika vipindi mbalimbali.
2.1.4.“Baraza la Kumbukumbu za Mikopo” maana yake ni baraza la kumbukumbu za mikopo lililoidhinishwa chini ya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania lililopo chini ya Kanuni ya Benki Kuu ya Tanzania (Baraza la Kumbukumbu ya Mikopo) ya mwaka 2012 miongoni mwa mambo mengine, kukusanya na kuwezesha uchangiaji wa taarifa za ukopaji za mteja;
2.1.5.“Mteja” maana yake ni mtu ambaye yuko katika kikundi ambacho jina lake liko katika akaunti ya M-KOBA iliyoko kwetu;
2.1.6.“Kituo cha Huduma kwa Mteja“ maana yake ni Maduka yoyote ya Rejareja ya Vodacom au vituo vingine vya rejareja kama vitakavyotaarifiwa kwa Mteja nasi katika vipindi mbalimbali;
2.1.7.“Fedha za Kielektroni” maana yake ni thamani ya fedha za kielektroni katika akaunti yako ya M-PESA zinazowakilisha thamani sawa na fedha taslimu;
2.1.8. “Kifaa” inajumuisha simu yako ya mkononi, Kadi ya SIMU na/ au vifaa vingine ambavyo vikitumika pamoja vinakuwezesha kupata Mtandao;
2.1.9.“MiddleWare” au “IPG” au “eKYC” maana yake ni mfumo uliowekwa na kuendelezwa na M-Pesa Limited ambao unaruhusu taarifa za mteja kuchangiwa kwa usalama na mtu mwingine aliyeidhinishwa (maana yake ni kampuni nyingine zote ambazo zinahusishwa na kitendo cha maombi ya mteja katika muktadha huu hasa inarejelea katika utaratibu wa M-Koba unaosimamiwa na sisi).
2.1.10.“Menyu ya M-KOBA” maana yake ni Menyu ya M-KOBA katika Mfumo wa M-PESA;
2.1.11.“Akaunti ya M-PESA” maana yake ni hifadhi ya thamani ya fedha zako katika simu ya mkononi, ambayo ni kumbukumbu iliyotunzwa na M-Pesa Limited ya kiwango cha Fedha za Kielektroni katika vipindi mbalimbali ikitunzwa na wewe katika Mfumo wa M-PESA;
2.1.12.“Huduma ya M-PESA” maana yake ni huduma ya uhamishaji wa fedha na malipo inayotolewa na Vodacom kupitia Mfumo wa M-PESA;
2.1.13.“Mfumo wa M-PESA” maana yake ni mfumo unaoendeshwa na M-Pesa Limited nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa Huduma ya M-PESA kwa kutumia Mtandao;
2.1.14.“Namba ya siri ya M-PESA“ maana yake ni namba ya utambulisho binafsi ambayo ni msimbo wa siri inayotumika kuingia katika Mfumo wa M-PESA na Akaunti yako ya M-KOBA;
2.1.15.“Mtumiaji wa M-PESA” maana yake ni mtu yeyote aliyesajiliwa kutumia Mfumo wa M-PESA kutuma, kupokea au kufanya malipo;
2.1.16. “Mtandao” maana yake ni mtandao wa simu ya mkononi unaoendeshwa na Vodacom PLC nchini Tanzania;
2.1.17.“Maombi” maana yake ni maombi au maelekezo yaliyopokelewa nasi kutoka kwako au kuelekezwa kutoka kwako kwa kutumia Mtandao na Mfumo na kupitia hayo tumeidhinishwa kufanyia kazi;
2.1.18.“Vodacom” maana yake ni Vodacom Tanzania PLC iliyoandikishwa nchini Tanzania kama kampuni yenye dhima yenye ukomo kwa umma chini ya Sheria ya Makampuni (Kifungu cha 486 cha Sheria za Tanzania);
2.1.19.“Huduma” itajumuisha aina yoyote ya huduma za benki au bidhaa ambayo tunaweza kutoa kwako kulingana na Mkataba huu na kama utakavyoitumia katika vipindi mbalimbali na “Huduma” itatafsiriwa ipasavyo;
2.1.20.“Kadi ya SIMU” maana yake ni mfumo wa utambulisho wa mtumiaji ambao unapotumika na simu ya mkononi inayohusika unakuwezesha kupata Mtandao na kutumia Mfumo wa M-PESA;
2.1.21.“Arafa” maana yake ni huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi unaotumwa kutoka katika simu moja ya mkononi kwenda katika simu nyingine au kutoka katika mfumo kwenda katika simu ya mkononi;
2.1.22.“Mfumo” maana yake ni programu ya kielektroni ya miamala ya kibenki na mawasiliano inayomwezesha mteja kuwasiliana na sisi kwa lengo la Huduma. Mfumo na Huduma kwa lengo la Mkataba huu utapatikana kupitia Mfumo wa M-PESA;
2.1.23.“Ada ya Muamala” inajumuisha ada na tozo zinazolipwa kwa ajili ya matumizi ya Huduma kama ilivyotangazwa nasi katika tovuti ya Benki na/ au tovuti ya Vodacom na/au magazeti ya kila siku ya Tanzania au kwa njia nyingine kama ambavyo Benki au M-Pesa Limited itakavyoona inafaa, hii inamaanisha kutakuwa na Tozo za M-Pesa na au za Benki;
2.1.24.“Urudishaji” maana yake ni kitendo cha kurudisha fedha kupitia Mtandao wa M-PESA ambazo ama zilikatwa au kuwekwa kwa makosa katika Akaunti ya M-KOBA;
2.1.25.“Sisi”, “yetu” na “nasi” maana yake ni Benki na M-Pesa Limited na, pale maudhui yanaporuhusu, inajumuisha warithi na walioteuliwa na Benki na Mpesa Limited;
2.1.26. “Wewe” au “yako” maana yake ni Mteja na inajumuisha wawakilishi binafsi wa Mteja.
2.1.27. “Mwenyekiti” maana yake ni mteja ambaye anaunda kikundi, pia mwanakikundi anayeidhinisha kutoa fedha katika akaunti ya kikundi ya M-KOBA kwenda katika akaunti ya Mteja ya M-Pesa, anamchagua katibu wa Kikundi na Mtunza Fedha wa Kikundi.
2.1.28.“Katibu” maana yake ni mwanakikundi ambaye anafanya muamala wa kuhamisha fedha kutoka katika akaunti ya M-KOBA kwenda katika Akaunti ya wanachama wa M-PESA.
2.1.29.“Mtunza Fedha” maana yake ni mwanakikundi ambaye anathibitisha muamala wa uhamishaji wa fedha kutoka katika akaunti ya M-KOBA hadi kwenye Akaunti ya M-PESA ya wanachama.
2.1.30.“Tukio lisilozuilika” maana yake ni kitu chochote kisichoweza kudhibitiwa na Upande wowote ikijumuisha magonjwa ya mlipuko, kuibuka kwa vita au ugaidi, uhamasishaji wa vurugu za kijeshi, vurugu au mgomo wa raia, majanga ya asili, tukio la viwandani au usumbufu kwa mfanyakazi (isipokuwa tukio la kiwandani litakalofanywa na wafanyakazi wa Upande wowote au waliopewa mkataba mdogo), zuio la fedha, kizuizi au kushindwa kwa huduma ya umma au chombo cha mawasiliano au kushindwa/kusitishwa kwa mfumo, usumbufu wakati wa kushughulikia muamala au ucheleweshaji unaotokana na tukio ambalo liko nje ya uwezo wetu (ikijumuisha kukatika kwa umeme na kucheleweshwa kwa mawasiliano na kituo cha mauzo cha msambazaji, intaneti au mfumo mwingine ikijumuisha kifaa chako kushindwa kufanya kazi).
2.1.31.“Mteja Asiyesajiliwa” maana yake ni mpokeaji au mtumaji wa Fedha za Kielektroni ambaye ni Mteja asiyesajiliwa kutoka kwa mtoaji mwingine wa huduma ya mtandao;
2.2.Neno “Mteja” litajumuisha jinsia zote ya kiume na ya kike pamoja na watu wa kisheria;
2.3.Maneno yanabeba maana ya umoja pale ambapo muktadha unakubali yatajumuisha maana ya wingi na kinyume chake.
2.4.Vichwa vya habari katika Kanuni na Masharti haya ni kwa malengo yanayofaa tu na haviathiri tafsiri ya Mkataba huu.
3.KUKUBALI KANUNI NA MASHARTI HAYA3.1.Kabla ya kuomba kufungua Akaunti ya M-KOBA kupitia Mfumo wa M-PESA unapaswa kusoma kwa makini na kuelewa Masharti ya Matumizi ambayo yataongoza matumizi na uendeshaji wa Akaunti ya M-KOBA.
3.2.Kama hukubaliani na Masharti ya Matumizi, tafadhali bofya “Decline – Kataa” katika menyu ya M-KOBA.
3.3.Utachukuliwa kuwa umesoma, umeelewa na umekubali Kanuni na Masharti haya: –
3.3.1.Baada ya kubofya katika chaguo la “Accept – Kubali” katika menyu ya M-KOBA inayokuhitaji kuthibitisha kuwa umesoma, umeelewa na umekubali kufuata Masharti ya Matumizi; na/au
3.3.2.Kwa kutumia au kuendeleza kutumia na kuendesha Akaunti ya M-KOBA.
3.4.Kwa kuomba kufungua Akaunti ya M-KOBA kwetu, unakubali kufuata na kuongozwa na Masharti ya Matumizi kwa sasa na katika vipindi mbalimbali kufuata taratibu zinazoongoza uendeshaji wa Akaunti ya M-KOBA na unathibitisha kwamba Masharti ya Matumizi yaliyomo humu hayavunji haki yoyote ambayo tunaweza kuwa nayo kwa kuzingatia Akaunti ya M-KOBA kisheria au vinginevyo.
3.5.Masharti ya Matumizi yanaweza kurekebishwa au kubadilishwa na sisi katika vipindi mbalimbali na kuendelea kutumia Akaunti yako ya M-KOBA kunamaanisha mkataba wako unafungwa na masharti ya marekebisho au mabadiliko yoyote.
3.6.Unakiri na kukubali kwamba tunatoa Akaunti ya M-KOBA kwa njia ya kielektroni tu na unakubali kufanya biashara na sisi na kuendesha Akaunti ya M-KOBA kwa njia ya kielektroni tu kupitia Menyu ya M-KOBA katika Mfumo wa M-PESA. Iwapo utakuwa na swali au malalamiko yoyote kuhusiana na Huduma yatashughulikiwa kwetu kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja. Ili kuepuka wasiwasi, unakiri na kukubali kuwa hutaruhusiwa wala kuwa na haki ya kupokea au kudai Huduma inayohusiana na Akaunti ya M-KOBA katika tawi lolote au matawi ya Benki au M-Pesa Limited isipokuwa kama itashauriwa na sisi kwa uamuzi wetu. Unakiri na kukubali kuwa Kituo cha Huduma kwa Mteja sio tawi la Benki au Wakala wa Benki kwa ajili ya kuendesha biashara au miamala ya Benki na kwamba haitafanya kazi hizo.
4.KUFUNGUA AKAUNTI4.1.Ili kufungua Akaunti ya M-KOBA kwetu, wanakikundi wote lazima wawe na umri wa angalau miaka 18 na Watumiaji waliosajiliwa na hai wa M-PESA. Benki pamoja na M-Pesa Limited ina haki ya kuthibitisha uhalali na hadhi ya Akaunti ya M-PESA ya wanakikundi.
4.2.Unaweza kufungua Akaunti ya M-KOBA mwenyewe kwa kutumia maombi ya kielektroni kwa kutumia Kifaa chako kwa kutumia Menyu ya M-KOBA katika Mfumo wa M-PESA.
4.3.Hapa unakubali na kuidhinisha Benki kuiomba M-Pesa Limited taarifa zako binafsi walizo nazo kulingana na Mkataba kati yako na M-Pesa Limited kwa ajili ya kupata bidhaa na huduma za M-Pesa Limited na Huduma ya M-PESA ikiwa ni pamoja na namba yako ya simu, jina, tarehe ya kuzaliwa, Namba ya Kitambulisho au Pasipoti na taarifa nyingine ambazo zitaiwezesha Benki kukutambua na kufuata mahitaji ya kimamlaka ya “Know Your Customer – Mjue Mteja Wako” (Kuzuia Utakatishaji wa Fedha) (pamoja na “Taarifa Binafsi”). Hapa pia unakubali na kuidhinisha Benki kuiomba M-Pesa Limited taarifa zinazohusiana na matumizi yako ya huduma ya M-PESA na Mfumo wa M-Pesa kama Benki itakavyohitaji kwa lengo la kukupatia Huduma (“Taarifa za M-PESA”). Hapa unaridhia kutolewa kwa Taarifa zako Binafsi na Taarifa za M-PESA zitakazotolewa na M-Pesa Limited kwa Benki na kwa matumizi yaliyoelezwa ya Taarifa Binafsi na Taarifa za M-PESA zitakazotolewa na Benki.
4.4.Hapa unakubali na kuidhinisha Benki kupata na kuzitumia Taarifa Binafsi zilizomo katika mfumo (kujumuisha lakini bila ukomo katika Middleware, IPG, eKYC n.k.) kutoka M-Pesa Limited na unakubali pia na kuridhia kutolewa kwa Taarifa hizo binafsi na M-Pesa Limited.
4.5.Hapa unakubali pia na kuidhinisha Benki kuthibitisha Taarifa zako Binafsi zilizopokewa kutoka M-Pesa Limited kwa mujibu wa Kifungu cha 4.3 dhidi ya taarifa zilizopokelewa kutoka M-Pesa Limited kama zilivyo katika MiddleWare/IPG, eKYC n.k.
4.6.Tuna haki ya kuomba taarifa zaidi kutoka kwako kuhusiana na maombi yako ya Akaunti ya M-KOBA wakati wowote. Kushindwa kutoa taarifa hizo katika muda unaotakiwa na sisi kunaweza kusababisha kukataliwa kwa maombi yako kwa ajili ya Akaunti ya M-KOBA.
4.7.Kukubalika na sisi kwa maombi yako kwa ajili ya Akaunti ya M-KOBA, kutafanyika kupitia arafa itakayotumwa kwenye Namba ya Simu ya Mkononi ya Vodacom iliyounganishwa na Akaunti ya M-PESA. Unakiri na kukubali kwamba kukubaliwa na sisi kwa maombi yako kwa ajili ya Akaunti ya M-KOBA kunatengeneza uhusiano wa kimkataba kati yako na sisi zaidi ya kanuni na masharti yanayotumika katika Akaunti yako ya M-PESA katika vipindi mbalimbali.
4.8.Tuna haki ya kukataa maombi yako kwa ajili ya Akaunti ya M-KOBA au kufuta maombi hayo katika hatua yoyote kwa uamuzi wetu kutokana na sababu itakayotolewa.
5.AINA YA AKAUNTIKama mmiliki wa Akaunti ya M-KOBA, kulingana na Masharti ya Matumizi, utakuwa na haki ya kuendesha akaunti ya kuweka amana ya M-KOBA (ambayo humu ni “Akaunti ya Akiba ya M-KOBA”) ambako unaweza kuhamishia fedha kutoka katika Akaunti yako ya M-PESA na/au kutoa fedha kutoka katika Akaunti ya M-PESA kutoka Benki kama ifuatavyo:
<>5.1.Akiba ya M-KOBA ya Familia/Marafiki5.1.1.Kama mwanakikundi wa Akaunti ya M-KOBA, unaweza kuweka amana kwenye Akaunti ya Akiba ya M-KOBA kwa kutumia Menyu ya M-KOBA katika Kifaa chako. Ada za kufanya miamala zinazolipwa kwa M-Pesa Limited kwa ajili ya miamala inayofanyika katika Akaunti yako ya M-Pesa katika vipindi mbalimbali itatumika katika miamala yoyote iliyofanyika katika Akaunti yako ya M-KOBA kwa kutumia Mfumo wa M-PESA.
5.1.2.Kuhamisha fedha nje ya akaunti ya kikundi kutafuata mchakato uliopangwa wa wanachama wa kikundi.
5.2.M-KOBA VICOBA/VSLA5.2.1.Kiongozi wa kikundi atapanga kiasi kilichokubaliwa na kikundi.
5.2.2.Kiongozi wa kikundi atapanga kiwango cha riba ya mkopo kwa mikopo iliyotolewa kutoka katika akaunti ya kikundi chao, na muda wa mkopo.
5.2.3.Wanakikundi wanaweza kutenga fedha za masuala ya kijamii (yaani, fedha ambazo Wanakikundi wameziweka kwa ajili ya masuala ya kijamii mfano, Harusi, Dharura, n.k.) kulingana na uamuzi wa wanakikundi.
5.2.4.Ulipaji (yaani ni mchakato wa kuhamisha fedha kutoka katika akaunti ya Mfuko wa Kijamii kwenda katika akaunti ya mwanakikundi) wa fedha za jamii kwa mwanakikundi unahusika na makato yoyote katika akaunti ya Ada ya Muamala unaohusika
5.2.5.Mwanakikundi anaweza kupata adhabu kulingana na uamuzi wa wanakikundi. Katibu anayehusika anaweza kupanga adhabu (yaani, Hizi ni jumla ya Tozo ambazo Wanakikundi wanapanga kwa ajili ya wanachama wao wanapokiuka kanuni zao za maadili walizokubaliana; mfano, kuchelewa kwenye vikao, kuchelewa kulipa mikopo. Adhabu zitafafanuliwa mapema na kikundi na kila kikundi kitakuwa na namna yake ya uendeshaji) ambapo hatua za kuidhinisha adhabu inafuatwa. Adhabu itakatwa kwanza kwa kila mchango.
6.ADA6.1.Umekubali kulipa Ada zote za Miamala inayolipwa kuhusiana na matummizi yako ya Huduma.
6.2.Utatulipa na tutakuwa na haki ya kukata kutoka katika Akaunti yako ya M-KOBA:
6.2.1.Ada zozote za Miamala zinazolipwa kulingana na Huduma;
6.2.2.Tozo zozote za kisheria zikijumuisha gharama za wakili na mteja zilizotumiwa na sisi katika kupata ushauri wa kisheria, usuluhishi au mashtaka mengine yaliyoibuka kutokana na shughuli yoyote kuhusiana na Akaunti yako ya M-KOBA; na
6.2.3.Ada nyingine zote, gharama na kodi, ushuru, tozo na gharama zilizotumika katika kushughulikia maombi yako.
6.3.Unakubali kulipa gharama zilizotumika na sisi katika kupata au kujaribu kupata malipo ya mkopo wowote unaodaiwa katika Akaunti yako ya Mkopo ya M-KOBA.
7.TAARIFA7.1.Unaweza kuomba taarifa au ripoti ya shughuli za Akaunti yako ya M-KOBA kutoka kwetu kwa kutumia Kifaa chako (“Taarifa fupi ya M-KOBA).
7.2.Taarifa Fupi ya M-KOBA itatoa maelezo ya kina ya miamala mitano (5) ya mwisho (au idadi nyingine ya miamala kama itakavyoamuliwa na sisi) katika Akaunti yako ya M-KOBA iliyofunguliwa katika Kifaa chako.
7.3.Taarifa Fupi ya M-KOBA haitatumwa kwako ikiwa imechapwa ila itakufikia ama kwa arafa katika Namba ya Simu ya Mkononi iliyounganishwa na Akaunti ya M-PESA au njia nyingine ya kielektroni kama tutakavyoamua kwa hiari yetu. Utawajibika kwa malipo na tozo zitakazotozwa na Vodacom wakati wa kufikisha kwako Taarifa Fupi ya M-KOBA
7.4.Unaweza kupata Taarifa Fupi za M-KOBA zilizochapwa au taarifa ya benki iliyochapwa inayohusiana na Akaunti yako ya M-KOBA kutoka katika Kituo cha Huduma kwa Mteja au maduka ya Vodacom. Utawajibika kwa malipo ya tozo zozote zilizotozwa na Kituo cha Huduma kwa Mteja au maduka ya Vodacom kwa ajili ya taaifa hizo zilizochapwa.
7.5.Hifadhi kwa ajili ya kosa la wazi, Taarifa Fupi ya M-KOBA au taarifa ya benki iliyotolewa kwako kama ilivyoelezwa awali kwa kuhusiana na Akaunti yako ya M-KOBA itaonyesha miamala iliofanyika katika Akaunti yako ya M-KOBA kwa kipindi kilichomo katika Taarifa Fupi ya M-KOBA na/au taarifa ya benki.
8.WAJIBU USIOBADILIKA8.1.Hapa unatuidhinishia sisi bila kubadilika kufanyia kazi Maombi yote yaliyopokelewa kutoka kwako (au kudai kutoka kwako) kupitia Mfumo na kukufanya uwajibike kuhusiana na hilo ombi, licha ya kwamba maombi hayo hayakuidhinishwa na wewe au hayahusiani na mamlaka yoyote yaliyopo yaliyotolewa na wewe.
8.2.Kama utatuomba sisi kusitisha muamala au maelekezo yoyote baada ya Maombi kupokelewa nasi kutoka kwako, kwa hiari yetu tutaweza kufuta muamala au maelekezo hayo lakini hatuwajibiki kufanya hivyo.
8.3.Tutakuwa na haki ya kupokea, kukubali na kufanyia kazi Maombi yoyote, hata kama Maombi hayo kwa sababu yoyote ile hayakukamilika au lina utata, kama kwa busara kabisa, sisi tunaamini kwamba tunaweza kurekebisha taarifa ambazo hazijakamilika au zenye utata zilizo katika Maombi bila taarifa kwako kuwa muhimu.
8.4.Sisi tumeidhinishwa kutekeleza maagizo yoyote yanayohusiana na Akaunti yako ya M-KOBA pale itakapohitajika kufanya hivyo kwa amri yoyote ya mahakama au mamlaka ya utendaji au chombo chochote chini ya sheria zinazotumika.
8.5.Kunapotokea mgogoro wowote kati ya masharti yoyote ya Maombi yaliyopokelewa na sisi kutoka kwako, basi Masharti ya Matumizi yatatumika.
9.VIFAA VYA MTEJA NA MAJUKUMU YA MTEJA.9.1.Kwa gharama zako utatoa na kutunza kifaa chako katika usalama na hali ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa madhumuni ya kupata Mfumo na Huduma.
9.2.Utawajibika kuhakikisha utendaji mzuri wa Kifaa chako. Hatuta husika/wajibika kwa makosa yoyote yanayotokana na uharibifu au kushindwa kufanya kazi kwa Vifaa vyako,na wala hatutawajibika kwa virusi vya kompyuta au matatizo yanayohusiana na hayo ambayo yanaweza kuhusishwa na matumizi ya Mfumo, Huduma na Kifaa. Utawajibika kwa tozo zitakazohusiana na mtoa huduma yeyote anayekuunganisha na Mtandao na hatutahusika kwa hasara au ucheleweshaji uliosababishwa na mtoa huduma huyo.
9.3.Unatakiwa kutafuata maelekezo yote, taratibu na masharti yaliyomo katika Kanuni na Masharti haya na waraka wowote uliotolewa na Benki na au M-Pesa Limited kuhusina na matumizi ya Mfumo na Huduma.
9.4.Unakubali na kukiri kuwa utahusika kikamilifu kwa ajili ya kutunza kwa usalama na matumizi mazuri ya Kifaa chako na kwa kutunza namba ya siri ya M-PESA kwa siri na usalama. Utahakikisha kwamba namba yako ya siri ya M-PESA haijulikani au kumilikiwa na mtu asiyeruhusiwa. Hatutahusika kwa uonyeshaji wowote wa namba yako ya siri ya M-PESA kwa mtu mwingine yeyote na hapa unakubali kulipa fidia na kutotusababishia madhara kwa upotevu wowote unaosababishwa na uonyeshaji wowote wa namba ya siri ya M-PESA.
9.5.Utachukua tahadhari zote muhimu kutambua/kugundua matumizi yoyote yasiyoidhinishwaya Mfumo na Huduma. Kwa hivyo , utahakikisha kwamba mawasiliano yote kutoka kwetu yanachunguzwa na kuhakikiwa na wewe au kwa niaba yako mara itakapowezekana baada ya kupokea kutoka kwako katika namna ambayo matumizi yoyote yasiyoruhusiwa ya upatikanaji wa Mfumo yatatambuliwa.
9.6.Utatufahamisha sisi haraka kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja inapotokea kwamba:
9.6.1.Una sababu ya kuamini kuwa namba yako ya siri (PIN) ya M-PESA inajulikana au inaweza kujulikana na mtu yeyote ambaye asiyeidhinishwa kuijua na/au / au kuathiriwa;; na/au
9.6.2.Una sababu ya kuamini kuwa matumizi yasiyoidhinishwa ya Huduma yamefanyika au yanaweza kufanyika au yangefanyika na muamala unaweza kuwa umefanyika kwa udanganyifu au kwa kukubaliana.
9.7.Wakati wote utafuata taratibu za usalama zitakazofahamishwa kwako na sisi katika vipindi mbalimbali au taratibu nyingine kama zitakavyotumika katika Huduma katika vipindi mbalimbali. Unakubali kwamba kushindwa kokote kwa upande wako kufuata taratibu za usalama zilizopendekezwa kunaweza kusababisha kuvunja usiri wa Akaunti yako ya M-KOBA. Kipekee, unaweza kuhakikisha kwamba Huduma haitumiki au maombi hayashughulikiwi au shughuli zinazohusika hazifanyiki na mtu yeyote zaidi ya mtu aliyeruhusiwa kufanya hivyo.
9.8.Wakati wowote huwezi na hautakiwi kuendesha au kutumia Huduma katika namna yoyote ambayo inaweza kuwa na madhara kwetu.
9.9.Wakati wowote utawajibika kwa muamala wowote utakaofanywa kwenda au kutoka katika Akaunti zako, na unathibitisha unatambua kuwa miamala ya M-KOBA hairudishwi/hairejeshwi.
9.10.Uhamishaji (yaani. Kutunza) au upokeaji wa fedha za kielektroni kwenda/kutoka akaunti ya M-KOBA kwa minajili ya Mteja Asiyesajiliwa (Mfano: Mteja kutoka kwenye mtandao mwingine kupitia mwingiliano wa kimtandao “aka. Interoperability“) kwa kutuma Maelekezo ya Kuhamisha/kupokea fedha kwenye Mfumo wa M-PESA kwenda/kutoka kwenye akaunti ya M-KOBA, ukihainisha kiasi kitakachohamishwa; kwa hali ya kuweka au kutoa au kupokea mkopo au kurejesha mkopo kama maelekezo ya mwombaji (Mteja Asiyesajiliwa) kutoka mtandao mwingine.
10.KUONDOLEWA KWA DHIMA/UWAJIBIKAJI WA MAMBO YASIYOJUMUISHWA10.1.Hatutawajibika kwa upotevu utakaosababishwa na wewe, kuingiliwa kwa huduma na au kutopatikana kwa sababu ya (a) kushindwa kwa kifaa chochote, au (b) mazingira mengine yoyote ambayo kwa namna yoyote hayako ndani ya uwezo wetu ikijumuisha, bila ukomo, matukio yasiyozuilika au kosa, kuingiliwa, kuchelewa au kutopatikana kwa Mfumo, ugaidi au kushindwa kwa kifaa kutokana na kitendo cha adui, kukosekana kwa nishati, hali mbaya ya hewa au angahewa, na kushindwa kwa mfumo wowote wa mawasiliano ya simu ya umma au binafsi.
10.2.Sisi hatutahusika kwa hasara au uharibifu utakaoupata kutokana na au kuhusiana na:
10.2.1.Kutopatikana kwa fedha za kutosha katika Akaunti yako ya M-PESA na/au katika Akaunti yako ya M-KOBA;
10.2.2.Kushindwa, kutofanya kazi vizuri, kuzuiliwa au kutopatikana kwa Mfumo wa M-Pesa na/au huduma ya M-Pesa, Kifaa chako na Mtandao;
10.2.3.Fedha katika Akaunti yako ya M-KOBA zikiwa katika mchakato wa kisheria au vikwazo vinavyozuia malipo au uhamishaji wake;
10.2.4.Kushindwa kwako kutoa maelekezo sahihi au yaliyokamilika kwa ajili ya malipo au uhamishaji unaohusiana na Akaunti ya M-KOBA;
10.2.5.Matumizi yoyote ya udanganyifu au yasiyo halali ya Huduma za M-Pesa, Mfumo wa M-Pesa na/au Kifaa chako; au
10.2.6.Kushindwa kwako kuzingatia Masharti ya Matumizi na nyaraka au taarifa zilizotolewa na Benki au M-Pesa Limited kuhusiana na matumizi ya Mfumo na Huduma.
10.3.Kama kwa sababu yoyote zaidi ya sababu zilizotajwa katika aya ndogo ya 10.1 au 10.2, Huduma imeingiliwa na au haipatikani, wajibu wetu chini ya Mkataba huu kuhusiana na hilo utakuwa kurejesha Huduma haraka iwezekanavyo.
10.4.Kama ilivyoelezwa katika kifungu kidogo cha 10.3 sisi hatutawajibika kwako kwa kuingiliwa kokote au kutopatikana kwa Huduma kwa sababu yoyote ile.
10.5.Kwa hali yoyote ile hatutawajibika kwako kwa sababu ya upotevu wa riba au akiba iliyotarajiwa au kwa upotevu wowote usio wa moja kwa moja au upotevu wenye madhara au uharibifu wa aina yoyote, uliosababishwa kwa namna yoyote, unaotokana na au kuhusiana na Huduma hata kama uwezekano wa upotevu au uharibifu huo umefahamishwa kwetu.
10.6.Vidokezo vyote/Dhamana zote na majukumu yote yaliyowekwa na sheria hapa yanaondolewa kulingana na kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria.
11.HAKI ZA MILKI YA UBUNIFUUnakubali kwamba haki za milki ya ubunifu ni Mfumo (na marekebisho yoyote, upandishaji hadhi au uimarishaji unaofanywa katika vipindi mbalimbali) na nyaraka zote zinazohusiana ambazo tunazitoa kwako kwa njia ya Mfumo au vinginevyo zinatolewa ama kwa Benki, M-Pesa Limited au kwa watu wengine ambao tuna haki ya kutumia au kutoa leseni kwa Mfumo na/au waraka uliotajwa. Hupaswi kukiuka haki zozote za milki ya ubunifu. Hupaswi kurudufu, kutoa nakala au kwa namna yoyote kuvuruga Mfumo na nyaraka zinazohusiana bila idhini yetu ya awali ya maandishi.
12.FIDIA12.1.Katika kutuzingatia sisi kufuata maelekezo au Maombi yako yanayohusiana na Akaunti ya M-KOBA, utatulipa fidia, kututoa katika madhara dhidi ya hasara yoyote, tozo, uharibifu, gharama, ada au madai ambayo tunaweza kupata au kuingia au kuendelea kupata na utatuondoa katika wajibu wote wa hasara au uharibifu ambao unaweza kuendelea kutoka kwetu kutokana na maelekezo au maombi yako au kutokana na Masharti ya Matumizi.
12.2.Fidia katika kifungu cha 12.1 itatumika pia katika yafuatayo:
12.2.1.Madai yote, hatua, hasara na upotevu wa aina yoyote ambao unaweza kuletwa dhidi yetu au ambao tunaweza kuupata au kuingia kutokana au kutotokana na Maombi au kuibuka kutokana na kutofanya kazi vizuri au kushindwa au kutopatikana kwa vifaa au programu, au kifaa, upotevu au uharibifu wa data yoyote, kukosekana kwa nishati, kuharibiwa kwa njia ya kutunzia, matukio ya asili, ghasia, kitendo cha uharibifu, hujuma, ugaidi, tukio jingine lolote lililo nje ya uwezo wetu, usumbufu au upotoshaji wa viungio vya mawasiliano au kuibuka kutokana na kumtegemea mtu yeyote au taarifa yoyote isiyokuwa sahihi, iliyo kinyume cha sheria, isiyo kamili au data zilizomo katika Maombi yoyote yaliyopokewa nasi.
12.2.2.Upotevu au uharibifu ambao unaweza kutokea kutokana na matumizi yako, matumizi mabaya, kudharau au kumiliki programu yoyote ya mtu mwingine yeyote, ikijumuisha lakini bila ukomo, katika mfumo wowote unaofanya kazi, programu ya kusakura au kifurushi chochote cha programu.
12.2.3.Ufikiaji/uingiaji wowote usioidhinishwa kwenye Akaunti yako ya M-KOBA au ukiukwaji/uvunjaji wowote wa usalama au uharibifu au upatikanaji wa data zako au uharibifu au wizi au uharibifu wa Kifaa chako chochote.
12.2.4.Hasara yoyote au uharibifu wowote unaotokana na kushindwa kwako kufuata Masharti ya Matumizi na /au kuwasilisha taarifa zisizo sahihi au upotevu au uharibifu unaosababishwa na kushindwa au kutopatikana kwa huduma au mifumo ya mtu mwingine au kutoweza kwa mtu mwingine kushughulikia muamala au upotevu mwingine wowote ambao unaweza kufanywa na sisi kama matokeo ya kukiuka Masharti ya Matumizi.
12.2.5.Uharibifu na gharama zitakazolipwa kwetu sisi kuhusiana na madai yoyote dhidi yetu kwa ajili ya kufidia upotevu ambao mazingira yake yapo ndani ya udhibiti wako.
13.MABADILIKO NA KUSITISHA MAHUSIANO.13.1.Sisi tunaweza wakati wowote, kukupa taarifa ya kusitisha kusitisha au kufanya mabadiliko ya uhusiano wetu wa kibiashara na wewe na hasa kufunga Akaunti yako ya M-KOBA lakini bila kuathiri ujumla wa yaliyotangulia. Tunaweza kusimamisha/ghahiri mikopo ambayo tunatoa na kudai marejesho ya malimbikizo madeni yaliyopo ambayo yametokana na muda huo kama tutakavyoamua. Aidha, unashauriwa kusoma, kuelewa na kufuata kanuni na masharti ya jumla ya GSM au ya huduma za Fedha kwa njia ya Simu ya Mkononi Kanuni na Masharti ya Mteja wa M-Pesa kwani yanaweza kusababisha kusitisha huduma kwa kukupa au kuto-kukupa taarifa, ingawa utakuwa na wajibu wa kulipa malimbikizo ya madeni yaliyopo.
13.2.Bila kuathiri haki zetu chini ya kifungu cha 13.1; kwa uamuzi wetu, baada ya kukufahamisha, tunaweza kusimamisha au kufunga Akaunti yako ya M-KOBA: –
13.2.1.Kama unatumia Akaunti ya M-KOBA kwa matumizi yasiyoruhusiwa au tutakapogundua matumizi mabaya, kukiuka maudhui, udanganyifu au kujaribu kufanya udanganyifu kuhusiana na matumizi yako ya Huduma;
13.2.2.Kama Akaunti yako ya M-PESA au mkataba na Vodacom au M-Pesa Limited umesitishwa kwa sababu nyingine yoyote;
13.2.3.Kama sisi tunatakiwa kufuata agizo au maelekezo au mapendekezo kutoka serikalini, mahakamani, kwa mdhibiti au mamlaka nyingine zenye sifa;
13.2.4.Kama kimsingi sisi tunashuku au kuamini kwamba unakiuka Masharti ya Matumizi (ikijumuisha kutolipa kiasi cha mkopo ulichopaswa kulipa ilipotakiwa);
13.2.5.Wakati ambapo usimamishaji au mabadiliko hayo ni muhimu kama matokeo ya matatizo ya kiufundi au kwa sababu za usalama;
13.2.6.Kuwezesha kuhuisha au kuboresha maudhui au ufanyaji kazi wa Huduma hiyo katika vipindi mbalimbali;
13.2.7.Wakati unapoendelea kutoitumia kwa kipindi cha muda ulioamuliwa na sisi kwa hiari yetu au kwa mahitaji ya kisheria; au
13.2.8.Kama sisi tutaamua kusimamisha au kusitisha utoaji wa Huduma kwa sababu za kibiashara au kwa sababu nyingine yoyote kama tutakavyoamua kwa hiari yetu.
13.3.Unaweza kufunga Akaunti yako ya M-KOBA wakati wowote katika Kituo chochote cha Huduma kwa Mteja.
13.4.Kama Akaunti yako ya M-KOBA ina deni lolote wakati wa kufungwa, tutarudisha salio hilo kwako, na tutakata ada yoyote inayotakiwa. Kama Akaunti yako ya Mkopo ya M-KOBA itakuwa na malimbikizo wakati wa kufunga Akaunti yako ya M-KOBA, unakubali kulipa haraka kiasi chote cha pesa unazodaiwa nasi.
13.5.Hata hivyo, kusimamishwa hakutaathiri haki na wajibu wowote wa upande wowote.
13.6.Kama nasi tukipokea taarifa ya kufariki kwako, hatutaruhusu uendeshaji au utoaji wa fedha kutoka katika Akaunti yako ya M-KOBA kufanywa na mtu yeyote isipokuwa kwa barua ya Usimamizi wa Mirathi au wawakilishi wako wa kisheria walioteuliwa kihalali na Mahakama.
14.UTOAJI WA TAARIFA14.1.Hapa unridhia/unakubali na kuidhinisha/kuturuhusu sisi kutoa taarifa, kupokea, kurekodi au kutumia taarifa zako binafsi au taarifa au data zinazohusiana na Akaunti yako ya M-KOBA/M-Pesa na taarifa za kina za matumizi yako ya Huduma:
14.1.1.Kwenda na kutoka kwa watekelezaji wowote wa sheria za nchi au za kimataifa au mamlaka yaliyoidhinishwa au vyombo vya serikali kwa kusisitiza katika uzuiaji na udhibiti, ugunduzi, uchunguzi au mashtaka ya vitendo vya uhalifu au udanganyifu;
14.1.2.Kwenda na kutoka kwa watoa huduma, wauzaji, mawakala, au kampuni nyingine yoyote ambayo unaweza kuwa au ni kampuni tanzu yetu au kampuni inayomiliki hisa kwa sababu za msingi za kibiashara zinazohusiana na Huduma;
14.1.3.Kwenda kwenye Baraza la Kumbukumbu ya Mikopo itakapohitajika;
14.1.4.Kwa wanasheria wetu, wakaguzi au washauri wa utaalamu mwingine kwa mahakama yoyote au mahakama ya usuluhishi kuhusiana na mashtaka yoyote ya kisheria au ya ukaguzi;
14.1.5.Kwa sababu za misingi ya kibiashara zinazohusishwa na matumizi yako ya Huduma, kama vile utafutaji wa masoko na shughuli zinazohusiana na utafiti; na
14.1.6.Katika utendaji wa biashara ukijumuisha bila kikomo katika udhibiti wa ubora, mafunzo na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa mfumo.
15.MAMBO MBALIMBALI15.1.Kanuni na Masharti haya (kama yanavyoweza kurekebishwa katika vipindi mbalimbali) yanaunda mkataba unaofunga kisheria kwako na kwa warithi wako.
15.2.Mkataba huu na haki zozote au dhima zilizopatikana humu haziwezi kutolewa na wewe kwa mtu mwingine yeyote.
15.3.Benki na au M-Pesa Limited inaweza kubadilisha au kurekebisha Kanuni na Masharti haya na ada za miamala wakati wowote na kukujulisha. Marekebisho au mabadiliko yoyote hayo yanaweza kuchapishwa katika mabango au vijitabu vitakavyopatikana katika vituo vya mawakala wa M-Pesa Limited, katika magazeti ya kila siku, Benki na/au katika Tovuti ya Vodacom/Benki na/au kwa njia nyingine yoyote kama itakavyoamuliwa nasi na mabadiliko au marekebisho hayo yoyote yataanza kutumika mara baada ya kuchapishwa au kutolewa taarifa kielektroni (Arafa/Mitandao ya Kijamii/ Programu Tumizi ya M-Pesa, n.k.)
15.4.Hakuna kushindwa au kucheleweshwa kutakakofanywa ama na wewe au sisi katika kutimiza haki au marekebisho yoyote kutakakoelezwa kutakakofanywa kama msamaha, wala zoezi lolote moja au la kawaida la utekelezaji wa sheria yoyote au marekebisho yatakayozuia kuendeleza au zoezi jingine lililopo au zoezi la haki au marekebisho mengine yoyote.
15.5.Haki na marekebisho yaliyopo yanatekelezwa kwa pamoja na bila kuacha haki au suluhisho lolote lililotolewa na sheria.
15.6.Kama kifungu chochote cha Masharti ya Matumizi kikionekana na msuluhishi aliyeteuliwa, mahakama au chombo cha usimamizi wa kimamlaka kuwa ni batili au hakitekelezeki, ubatili au kutotekelezeka kwa kifungu hicho hakutaathiri vifungu vingine vilivyomo.
16.TAARIFA16.1.Tunaweza kutuma taarifa kuhusiana na Akaunti ya M-KOBA kwa arafa au kwa ujumbe (USSD push) katika namba ya Simu ya Mkononi ya Vodacon iliyounganishwa na Akaunti yako ya M-PESA.
16.2.Unakubali kwamba huna madai dhidi yetu kutokana na hasara iliyosababishwa na upotevu, ucheleweshaji, kutoelewana, kuondolewa kwa sehemu muhimu, urudiaji au kutokuwapo kwa usawa wowote kutokana na usambazaji wa mawasiliano yoyote yanayohusiana na Akaunti ya M-KOBA
17.UTATUZI WA MIGOGORO NA MAMLAKA YA KISHERIA17.1.Unaweza kuwasiliana na sisi kupitia namba 100/101 ya kituo cha huduma kwa mteja au mawasiliano mengine ya kituo cha huduma kwa mteja yaliyotolewa katika mitandao ya kijamii au Tovuti (yaani, TOBi Mtandaoni au Wasilisha maswali) kuripoti migogoro yoyote, madai au hitilafu katika Huduma.
17.2.Wawakilishi wetu wa huduma kwa mteja watashughulikia jambo lililoripotiwa kulingana na viwango vyetu vya taratibu za kushughulikia malalamiko.
17.3.Simu zinazopigwa kituoni zinaweza kurekodiwa kwa ajili ya kuhakikisha ubora au kwa ajili ya utendaji wa kibiashara ikijumuisha bila kikomo katika udhibiti wa ubora, mafunzo na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa mifumo.
17.4.Kutusaidia sisi tukuhudumie vizuri, tafadhali tuletee taarifa zako sahihi zinazohusiana na malalamiko yako (mf. tarehe & muda wa tukio, bidhaa, taarifa za kina za mtu yeyote uliyezungumza naye kuhusiana na malalamiko, n.k.).
17.5.Mchakato wa kushughulikia malalamiko ni bure.
17.5.1.Malalamiko ya Fedha kwa njia ya Simu – kama malalamiko yako yanayohusiana na fedha kwa simu ya mkononi hayakutatuliwa kwa kiwango cha kuridhisha ndani ya siku 21 tangu yalipopokewa na Vodacom, una haki ya kupeleka malalamiko yako Benki Kuu ya Tanzania kwa kufuata utaratibu ufuatao:
17.5.1.1.Hatua ya 1: Fungua katika Tovuti ya BoT: https://www.bot.go.tz kupata Fomu ya Malalamiko ya BOT
17.5.1.2.Hatua ya 2: Tuma Fomu ya Malalamiko BoT kwa njia yoyote kati ya zifuatazo:
17.5.1.2.1.Kwa Mkono: Kitengo cha Mtumiaji wa Fedha, Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Makao Makuu, 2 Mtaa wa Mirambo, Dar es Salaama, ghorofa ya chini, Jengo la katikati.
17.5.1.2.2.Kwa Njia ya Posta: Kitengo cha Mtumiaji wa Fedha, Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Makao Makuu, S.L.P. 11884, Dar es Salaam,
17.5.1.2.3.Kwa Faksi/ Kwa facsimile: +255 22 2234067
17.5.1.2.4.Kwa simu: +255 22 2233265/ +255 22 2233246
17.5.1.2.5.Kwa Baruapepe, Ainoe Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Mtumiaji wa Fedha yaani. [email protected]
17.5.1.2.6.Kwa tovuti (Mtandaoni) https://www.bot.go.tz
17.5.2.Malalamiko ya Fedha kwa Njia ya Simu – kama malalamiko yako yanayohusiana na fedha kwa njia ya simu ya mkononi hayakutatuliwa kwa kiwango cha kuridhisha kwa malengo au upitiaji wa malengo unaofanywa na Benki Kuu ya Tanzania, Mteja anaweza kuomba upitiaji wa kisheria wa Mahakama.
17.5.3.Malalamiko ya GSM: – kama malalamiko yako hayakutatuliwa kwa kiwango cha kuridhisha ndani ya siku 30 tangu yalipoletwa Vodacom, una haki ya kupeleka malalamiko yako kwenye Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania kwa kufuata utaratibu ufuatao:
17.5.3.1.Hatua ya 1: Ingia katika Tovuti ya TCRA: www.tcra.go.tz kupata Fomu ya Malalamiko ya TCRA
17.5.3.2.Hatua ya 2: Tuma Fomu ya Malalamiko ya TCRA kwenda TCRA kwa njia mojawapo kati ya zifuatazo:
17.5.3.2.1.Kwa Mkono: Idara ya Masuala ya Mtumiaji ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano, Mawasiliano Towers, Kitalu Na. 2005/1, Kiwanja C, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam
17.5.3.2.2.Kwa njia ya Posta: Idara ya Masuala ya Mtumiaji ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA) Towers, S.L.P 474, Dar es Salaam
17.5.3.2.3.TCRA- Kwa Faksi: +255 22 2412009/10
17.5.3.2.4.TCRA- Kwa Baruapepe: [email protected]
17.5.3.2.5.TCRA- Tovuti (Mtandaoni): www.tcra.go.tz
17.5.4.Malalamiko ya GSM: – kama malalamiko yako hayakutatuliwa na TCRA kwa kiwango cha kuridhisha, una haki ya kupeleka malalamiko yako kwenye Mahakama ya Usuluhishi ndani ya siku 21 baada ya uamuzi wa TCRA kwa kufuata utaratibu ufuatao:
17.5.4.1.Hatua ya 1: Ingia katika Tovuti ya FCC: www.competition.or.tz kupata Fomu ya Malalamiko ya FCC
17.5.4.2.Hatua ya 2: Tuma Fomu ya Malalamiko ya FCC kwenda FCC kwa moja kati ya njia zifuatazo:
17.5.4.2.1.Kwa mkono: Tume ya Ushindani wa Biashara, Jengo la GEPF, Ghorofa ya 2, Kiwanja Na. 37, Regent Estate Barabara ya Bagamoyo, Dar es Salaam.
17.5.4.2.2.Kwa njia ya Posta: Tume ya Ushindani wa Biashara, Jengo la GEPF, S.L.P 7883, DSM, Tanzania
17.5.4.2.3.Kwa Faksi: +255 22 2926126
17.5.4.2.4.Kwa Baruapepe: [email protected]
17.5.4.2.5.Kwa Tovuti (Mtandaoni): www.competition.or.tz
17.6.Unaweza kuwasiliana na Kituo cha Huduma kwa Mteja kuripoti migogoro, madai au hitilafu yoyote katika Akaunti ya M-KOBA.
17.7.Masharti ya Matumizi yatasimamiwa na kutumika kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tags: KANUNI na Masharti ya Kufungua na Kutumia Akaunti ya M-KOBA