KANUNI za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024
KANUNI za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024
KANUNI za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024KANUNI za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024,Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024.
Kanuni hizi zitatumika katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo-
- Afisa Mwandikishaji maana yake ni mtu aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria na inajumuisha afisa mwandikishaji msaidizi;
- Afisa wa Tume maana yake ni mwajiriwa wa Tume;
- Chama cha Siasa maana yake ni chama cha siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa;
- Daftari maana yake ni Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoanzishwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria;
- Daftari la Awali la Wapiga Kura maana yake ni daftari
lililoanzishwa chini ya kifungu cha 11 cha Sheria; - jimbo maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni ya uchaguzi wa Mbunge;
- Kadi ya Mpiga Kura maana yake ni kadi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria, ikithibitisha kwamba mtu aliyetajwa katika kadi hiyo ameandikishwa kuwa mpiga kura;
- Katiba maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977;
Tags: KANUNI za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024