LAMECK Lawi ni Mnyama
LAMECK Lawi ni Mnyama
LAMECK Lawi ni Mnyama,Beki kisiki wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Lameck Lawi anasubiri utambulisho tu pale Msimbazi.
Ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu ya Simba kufikia makubaliano ya kumnunua kutoka Katika Klabu yake ya Coastal Union Tanga.
Lawi alikuwa Jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwaajili ya kusaini Mkataba na baada ya kukamilisha zoezi hilo, alirejea Tanga kujiunga na timu yake kwaajili ya kuendelea na maandalizi ya mechi zilizobaki
Mmoja wa viongozi waandamizi wa klabu ya Simba alithibitisha kuwa tayari usajili wa Lawi wameukamilisha na mchezaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao
“Tumemaliza na Lawi wa Coastal Union baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufikia makubaliano, Ni beki mzuri hatuna shaka na uwezo wake, kwani hata kocha Juma Mgunda ameridhishwa naye kwa sababu ni mchezaji ambaye amepita chini yake amesisitiza asajiliwe”
“Lawi tayari kasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba msimu ujao tunaamini atafanya kazi nzuri kama ilivyo sasa ndani ya kikosi cha Coastal Union,” alisema
Katika msimu huu Lawi ameiongoza Coastal Union akiwa na nahodha ambapo wagosi hao wa Kaya wako nafasi ya nne katika Msimamo wa Ligi na wanapambana kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao.
Coastal Union pia iko hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la CRDB ambapo itachuana na Azam FC May 18 kuwania kutinga Fainali hiyo ya CRDB Bank Federation Cup 2023/2024.
Tags: LAMECK Lawi ni Mnyama