MABADILIKO ya Ratiba ya SGR Dar to Moro Kuanzia July 05-2024
MABADILIKO ya Ratiba ya SGR Dar to Moro Kuanzia July 05-2024
MABADILIKO ya Ratiba ya SGR Dar to Moro Kuanzia July 05-2024z Shirika la Reli Tanzania limetangaza ongezeko la safari za treni ya kisasa (SGR) zitakazohusisha kuanza kwa treni mpya ya mwendo kasi (Express train) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro bila kusimama vituo vya kati.
Ratiba iliyotolewa inaonyesha kutakuwa safari nane kwa siku na treni hizo zitakuwa zinapishana kwa takribani dakika 20 kati ya treni ya kawaida na ile ya mwendokasi.
Ongezeko la safari hizo limekuja ikiwa siku 16 zimepita tangu kuanza kwa safari za treni hiyo ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo zilikuwa safari nne kwa siku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRC Jumatatu Julai mosi, 2024, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk mabadiliko hayo yataanza rasmi Julai 5, 2024.
Mabadiliko ya ratiba yatakuwa kama ifuatavyo; Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku. Treni itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 1:30 usiku.
Pia, treni ya kawaida itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na itaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.
Aidha TRC imewashauri abiria kukata tiketi kwa njia ya mtandao au madirisha ya tiketi yaliyo ndani ya vituo vya treni saa 2 kabla ya muda wa safari, ili kuepuka Msongamano.
Tags: MABADILIKO ya Ratiba ya SGR Dar to Moro Kuanzia July 05-2024