MAJINA 115 ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Chato 18-05-2024
MAJINA 115 ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Chato 18-05-2024
MAJINA 115 ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Chato 18-05-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Chato Leo tarehe 18 May 2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Chato May 182-204.
- MAJINA 232 ya Waliotwa kwenye Usaili Wilaya ya Mbarali 18-05-2024
- MAJINA 418 ya Waliotwa kwenye Usaili Wilaya ya Biharamulo 18-05-2024
- MAJINA 566 ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Bunda 18-05-2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote
walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 25-05-2024 hadi 26-05-2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye
usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika. - Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO LEO MAY 18-2024
MAJINA 115 ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Chato 18-05-2024
HISTORIA FUPI YA WILAYA YA CHATO
Chato ni mojawapo ya Wilaya tano za Mkoa wa Geita na ilianzishwa rasmi Julai 2006 kutokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Biharamulo.
Wilaya ya Chato ina Halmashauri moja yaani Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyoanzishwa rasmi Julai, 2007.
MIPAKA NA ENEO LA WILAYA
Wilaya ya Chato ipo Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kati ya Latitudo 20 15’ hadi 30 15’ Kusini mwa Ikweta na Longitudo 310 hadi 32o Mashariki ya Greenwich.
Wilaya inapakana na Wilaya ya
Muleba Kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Bukombe kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Biharamulo kwa upande wa Magharibi na Wilaya ya Geita kwa upande wa Mashariki.
Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 3,572 na iko kwenye mwinuko wa kati ya meta 1,135 hadi 1,410 kutoka usawa wa bahari.
IDADI YA WATU
Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na idadi ya watu 365,127 ambapo kati ya hao 181,368 ni Wanaume na 183,759 ni Wanawake. Idadi ya kaya ni 60,855 sawa
na wastani wa watu 6 kwa kaya.
Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapato 175,261 sawa na asilimia 48 ya wakazi wote. Hadi kufikia 31 Desemba, 2017 Wilaya inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 420,191 wanaume ni 208,720 na wanawake ni 211,471 (Chanzo cha taarifa NBS )
UTAWALA
Kiutawala Wilaya ya Chato imegawanyika katika Tarafa 5 za Buzirayombo, Bwanga, Buseresere,
Kachwamba na Nyamirembe. Kuna Kata 23 zenye Vijiji 115 na Vitongoji 599. Makao Makuu ya Wilaya ni Chato.
Wilaya ina jimbo moja la uchaguzi, Madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa
kuchaguliwa kwenye Kata na 8 ni wanawake kupitia viti maalum na Mhe. Mbunge 1.
Tags: Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Chato Leo tarehe 18 May 2024, MAJINA 115 ya Waliotwa kwenye Usaili Wilaya ya Chato 18-05-2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Chato May 182-204, TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO 18-05-2024.