MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili TET August 2024
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili TET August 2024
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili TET August 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) anapenda kuwataarifu waombaji waliokidhi vigezo katika tangazo la Ajira ya Mkataba nafasi ya MKUZA MITAALA SOMO LA UTALII (TOURISM).
Waombaji waliokidhi vigezo wanataarifiwa kuwa usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29/08/2024 hadi 30/08/2024 saa mbili Kamili Asubuhi katika Ofisi za Makao Makuu ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zilizopo Mwenge- Bamaga Karibu na Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Kila Msailiwa anatakiwa kufika akiwa amevaa NADHIFU.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (ORIGINAL), kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI na Shahada.
- Wasailiwa watakaowasilisha (Testimonials, Provisional Results, Statement of results) hati za matokeo HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
- Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kufika na Hati za Uhakiki wa Vyeti vyao kutoka kwa Mamlaka zinazohusika (kama TCU, NACTE au NECTA).
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa kwa kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA