RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 09/04/2024

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa April 2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa April 2024, Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Mpwapwa April 2024,TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA 09-04-2024.

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa April 2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa April 2024, Majina ya Waliotwa Kwenye Usaili Mpwapwa April 2024,TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA 09-04-2024.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote
walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 17.04.2024 – 18.04.2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili
wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe 17.04.2024 hadi tarehe 18.04.2024 kama ilivyooneshwa kwenye
    tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
    kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
    Astashahada.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
    HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
    vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
  • Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Wilaya ya Mpwapwa ni ya joto . Hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazoendana na hali hiyo.

KUONA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA 09-04-2024 DOWNLOAD PDF HAPA

Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

Jiografia  ya wilaya ya Mpwapwa

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa Halmashauri nane (8) za Mkoa wa Dodoma. Makao makuu yapo umbali wa km.120 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Dodoma.

Halmashauri ipo kati ya latitude 6°00” na 7°00” Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudo 35°45” na 35°00” Mashariki mwa mstari wa ‘Greenwich’.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa upande wa magharibi. Upande wa mashariki inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (mkoa wa Morogoro) na kusini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Mkoa wa Iringa).

Ukubwa wa eneo 

Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 7,479 sawa na (18.35%) ya eneo lote la Mkoa wa Dodoma.  Eneo hili ambalo ni sawa na hekta 737,900 linatumika kwa shuguli za kilimo, ufugaji, hifadhi ya misitu na makazi

Muundo wa Halmashauri ya Wilaya Kiutawala

Halmashauri ya Wilaya ina Majimbo 2 ya Uchaguzi, Tarafa 4, Kata 33, Vijiji 113, Vitongoji 575 na Mitaa 18.

 Idadi ya Watu

Kutokana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ya Wilaya ilikadiriwa kuwa na wakazi 305,056 ambapo Wanaume wakiwa 147,306 (48.3%), Wanawake 157,750 (51.7%) na Kaya 66,316. Aidha, kwa mwaka 2016 kwa kutumia ukuaji wa asilimia 2.1, inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 331,500 kati yao Wanaume 162,435, na Wanawake 169,065 wanaoishi katika Kaya 72,065. Mgawanyo wa idadi ya watu kitarafa kwa ulinganisho wa Idadi ya Watu Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2012 na makadirio ya watu mwaka 2016.

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Mpwapwa 09-04-2024

Tags: , , , ,

Comments are closed.