MASWALI Yanayoulizwa Mara Kwa Mara Ajira za INEC
1:Nini kitatokea ikiwa mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja?
Jibu: Ni kosa la jinai mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja, na ikitokea, mtu ataadhibiwa kulingana na sheria za Uchaguzi.
2:Je Mawakala wa vyama vya Siasa wanaruhusiwa kuangalia zoezi la uandikishaji wapiga kura kituoni?
Jibu: Ndio, Mawakala wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wanaruhusiwa kuwa na mwangalizi mmoja kwa kila kituo cha Uandikishaji Wapiga kura.
3:Kwa nini Ujiandikishe kuwa Mpiga Kura?
Jibu: Ili kuweza kutimiza haki yako katika Kupiga Kura siku ya Kura ya Maoni na Uchaguzi, Kuweza kushiriki katika uongozi Nchi yako.
4:Nani anapoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga kura?
Jibu: Ikiwa ana Uraia wa Nchi nyingine yaani sio Raia wa Tanzania, Amehukumiwa kifungo cha zaidi ya Miezi Sita, Amehukumiwa kifo na Mahakama za Tanzania, Amethibitika kuwa hana Akili timamu.
5:Uteuzi ni nini?
Jibu: Uteuzi ni sehemu ya Mchakato wa Uchaguzi, ambapo Tume inamteua Mgombea Kugombea nafasi katika Uchaguzi. Mgombe huyo ni sharti awe ameteuliwa na chama chake cha Siasa.
- Afisa Mwandikishaji maana yake ni mtu aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria na inajumuisha afisa mwandikishaji msaidizi;
- Afisa wa Tume maana yake ni mwajiriwa wa Tume;
- Chama cha Siasa maana yake ni chama cha siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa;
- Daftari maana yake ni Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoanzishwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria;
- Daftari la Awali la Wapiga Kura maana yake ni daftari
lililoanzishwa chini ya kifungu cha 11 cha Sheria; - jimbo maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni ya uchaguzi wa Mbunge;
- Kadi ya Mpiga Kura maana yake ni kadi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria, ikithibitisha kwamba mtu aliyetajwa katika kadi hiyo ameandikishwa kuwa mpiga kura;
- Kata maana yake ni mgawanyo wa mamlaka katika mamlaka za serikali za mitaa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji);
- Kiapo cha kutunza siri maana yake ni kiapo kinachozuia kutoa taarifa yoyote ya mtu aliyeomba kuandikishwa au jambo lolote linalohusu uandikishaji isipokuwa kwa madhumuni yaliyoidhinishwa kwa mujibu wa sheria
- kijiji itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya)
- Kitongoji itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya);
- Kituo Cha Uandikishaji maana yake ni kituo kilichoanzishwa na Tume kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura;
- Mfungwa itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Magereza na kwa madhumuni ya Kanuni hizi, inajumuisha mahabusu Sheria Na. 2 ya Mwaka 2024
- Mkurugenzi wa Uchaguzi itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi; Sura ya 288
- Mtaa itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika
Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); - Mwangalizi Wa Uandikishaji maana yake ni mwangalizi wa uandikishaji wa ndani au wa kimataifa aliyeidhinishwa na Tume;
- Mwandishi Msaidizi maana yake ni mtu aliyeteuliwa na afisa mwandikishaji chini ya kanuni ya 11 na itajumuisha mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki;
- Namba ya kipekee ya utambuzi wa mpiga kura maana
yake ni namba ya kudumu ya utambulisho wa mpiga kura. - Taarifa za uandikishaji maana yake ni taarifa za mpiga kura zilizoandaliwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria;
- Tume maana yake ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
- Uboreshaji maana yake ni uandikishaji wa wapiga kura wapya wenye sifa, ufanyaji wa marekebisho ya taarifa za wapiga kura, uhamishaji wa taarifa za wapiga kura, utoaji wa kadi mpya kwa wapiga kura na ufutaji wa majina ya waliopoteza sifa kwenye
Daftari uchaguzi maana yake-
(a) iwapo ni kumchagua Rais, ni uchaguzi wa Rais;
(b) iwapo ni kumchagua Mbunge, ni uchaguzi wa Mbunge, na inajumuisha uchaguzi mdogo; na
(c) iwapo ni kumchagua Diwani, ni uchaguzi wa
Diwani, na inajumuisha uchaguzi mdogo;
- Vifaa Vya Uandikishaji maana yake ni vifaa vilivyopata kibali cha Tume kwa lengo la kutumika katika
uandikishaji
Wakala Wa Uandikishaji maana yake ni mtu aliyeteuliwa na chama cha siasa kuwa wakala chini ya kifungu cha 17 cha Sheria; na
Watendaji Wa Uandikishaji inajumuisha mratibu wa
uandikishaji wa mkoa, afisa mwandikishaji, afisa mwandikishaji msaidizi, mwandishi msaidizi,
mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki na watendaji wengine watakaoteuliwa na Tume.
SOMA NA HII:
Tags: Maswali ya Interview Ajira za INEC, Maswali ya Interview Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, MASWALI Yanayoulizwa Mara Kwa Mara Ajira za INEC, Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara Ajira za NEC., Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara Ajira za INEC
Nimependa sana ukurasa wenu
Karibu
Nimefurahi kuona maelekezi mazuri kuusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
Karibu
Nimepata maarifa zaidi
Asante sana kwa taarifa sahihi na nzuri yenye kutuongezea fikra chanya juu ya INEC……
SWALI JE MAJINA MENGINE YA MIKOA MINGINE YA WALIOOMBA USIMAMIXI WA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA YANATOKA LINI MAANA TUNAONA YA KIGOMA TU????
Yatatoka tu, yameanza ya Kigoma Kwa sababu ndipo Uzinduzi utafanyika July Mosi
Ahsanteni kwa ufafanuzi mzuri hakika nimepata maarifa zaidi