RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MULEBA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO MWAKA WA FEDHA 2023-2024

Filed in Habari by on 21/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ya Mkoani Kagera imevuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani kwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 8.6 sawa na asilimia 125 ya lengo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

MULEBA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO MWAKA WA FEDHA 2023-2024

MULEBA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO MWAKA WA FEDHA 2023-2024

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe.Magongo Justus amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya nne ambacho kimefanyika Agosti 16 mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Mhe.Magongo amesema kuwa awali walikuwa wamelenga kukusanya shilingi bilioni 6.5 hivyo kutokana na ushirikiano wa Madiwani na watumishi wa Wilaya wameweza kuvuka lengo na fedha hizo zimeenda kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tulipanga kukusanya na kutumia Bilion 6.5 lakini tumefanikiwa kukusanya bilioni 8.6 ambayo ni sawa na asilimia 125 jambo ambalo limepelekea kutekeleza miradi mbalimbali katika ngazi zetu za kata na vijiji lakini pia kuindesha halmashauri yetu”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amelitaka baraza la madiwani kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Pia amewataka madiwani kusimamia swala la lishe mashuleni ili kuondoa hali ya udumavu kwa watoto ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi.

“watoto wetu huko wanasoma kuanzia asubuhi mpaka jioni hawajapata chakula jambo hili lazima tulikatae sote na tuseme watoto wetu, wazazi wetu huko wachangie chakula kwa watoto wetu ili wasome katika mazingira rafiki”

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa taasisi, Kamati ya usalama ya wilaya na viongozi wa dini.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.