NAFASI 105 za Afisa Kilimo MDAs na LGAs August 2024
NAFASI 105 za Afisa Kilimo MDAs na LGAs August 2024
NAFASI 105 za Afisa Kilimo MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 105 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.
✅AFISA KILIMO DARAJA LA II (NAFASI 105)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;
- Kukusanya takwimu za bei na mazao kila wiki na kila mwezi;
- Kukusanya takwimu za upatikanaji mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi;
- Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo;
- Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana;
- Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara;
- Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji;
- Kutoa habari juu ya technolojia mpya kwa wadau;
- Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao;
- Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine;
- Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora;
- Kuandaa, kutayarisha, kufunga na kusambazambegu bora
SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wenye Shahada ya Kilimo au Shahada ya Sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani TGS D.
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama
ifuatavyo;.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
Cheti cha kuzaliwa - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
Tags: 105 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024., MDAs & LGAs August 2024, MDAs & LGAs Jobs, NAFASI 105 za Afisa Kilimo MDAs na LGAs August 2024