RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Mufindi July 2024

Filed in Ajira by on 24/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Mufindi July 2024

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Mufindi July 2024

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Mufindi July 2024

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Mufindi July 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya Mufindi kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb.Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 na kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA. 228/613/01/C/068 cha tarehe 12 Juni 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 5)

KAZI NA MAJUKUMU.

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoing correspondence register);
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officer);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
  • Kutafuta  kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) na mahali pegine yanapohifadhiwa;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking); na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mwajiri au Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye Stashahada au NTA Level 6
katika fani ya Utunzaji kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS C

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 13)

KAZI NA MAJUKUMU.

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji.
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji.
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
  • Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji.
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
  • Mwenyekiti wa kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au kidato cha Sita (VI).
Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS B.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia usiozidi miaka 45
    isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
    kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya
    Taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanaliyojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • “Testimonials, Provisional results, Statement of results” havitakubaliwa.
    Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
    Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 04/08/2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,
S.L.P 223,
MAFINGA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: http://portal.ajira.go.tz anuani hii inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment
Portal”.

Maombi yatakayowasilishwa nje utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.