NAFASI 27 za Kazi Wilaya ya Kasulu July 17-2024
NAFASI 27 za Kazi Wilaya ya Kasulu July 17-2024
NAFASI 27 za Kazi Wilaya ya Kasulu July 17-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu amepokea kibali cha Ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na. FA.228/613/01/C/021 cha tarehe 20 Mei, 2024 na kibali chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni 2024.
Hivyo watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA II – NAFASI (2),
MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya mishahara ya Serikali TGS B.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II NAFASI 4
MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa
- Kutunza taarifa za kumbukumbu za matukio,miadi,tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine
- Kutafuta majalada,nyaraka zinazohitajika katika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/ Kitengo/ Sehemu husika
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi na
- Kufanya kazi zingne atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mshahara wa serikali TGS C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II- NAFASI 1
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (Incoming correspondence register)
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (Outgoing correspondence register)
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi Masijala toka kwa watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada 9Racks/Filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi ( File tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinatyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGS C.
✅MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI 20
KAZI NA MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA MUOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha kidato cha Nne (IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zAwe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheia, Elimu ya jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au chochote kinachotambulika na Serikali
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa Kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Diploma/Certificate, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma.
- Testimonials, “Provision Results”, “Statements of Results”, hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/07/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya
S.L.P 97
KASULU
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 20 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu More Details |
2024-07-30 Login to Apply |