RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 47 za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke July 12-2024

Filed in Ajira by on 12/07/2024

NAFASI 47 za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke July 12-2024

NAFASI 47 za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke July 12-2024

NAFASI 47 za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke July 12-2024

NAFASI 47 za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke July 12-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Temeke kuomba nafasi za kazi ziliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma naUtawala Bora.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE 12-07-2024

✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA III (NAFASI 42)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa masuuli na Mtendaji mkuu wa Serikali ya kijiji;
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, Kuwa mlinzi wa Amani na usimamizi wa Utawala Bora katiaka kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi
    katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika kijiji;
  • Kusimamia, Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchiKusimamia utungaji wa Sheria ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada (Cheti) NTA Level 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya mshahara wa Serikali TGS B.
1.2

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI 05

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kufanya usafi wa Gari
  • Kufanya kazi nyigine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18
    na usiozidi miaka 45;
  • Waomabji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuaninisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/ Wakili;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
    (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne,
    Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Testmonials Provisional Results Statement of Rusults hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji walisoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE)
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji watakao wasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za
    kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24/07/2024

Muhimu: Kumbuka Kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamaoja na vyeti vya elimu.Barua zote za maombi ziandikwe kwa;
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,
S. L. P 46343,
DAR ES SALAM.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘
“Recruitment Portal’

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATASHUGHULIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.