RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024

Filed in Ajira by on 28/06/2024

NAFASI 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024

NAFASI 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024

NAFASI 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024

NAFASI 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024, Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini unatangaza nafasi 54 za Ajira ya Mkataba wa kujitolea kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) kama ifuatavyo: –

✅Daktari Bingwa Daraja la II – (NAFASI 02)
KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini
MASHARTI YA AJIRA: Kujitolea, Mkataba wa Mwaka 1

SIFA
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

KAZI: Daktari Bingwa
MWAJIRI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MUDA WA MAOMBI: 28/06/2024 – 14/07/2024

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya kazi zote za matibabu ya Kibingwa.
  • Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
  • Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
  • Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake
  • Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement)
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

MSHAHARA NA POSHO
Malipo ya mshahara yatazingatia Mwongozo wa Afya wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline). Aidha posho nyingine zitalipwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

✅Daktari Daraja la II – (NAFASI 09)

KITUO CHA KAZI:Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini
MASHARTI YA AJIRA:Kujitolea, Mkataba wa Mwaka 1

SIFA
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

KAZI: Daktari
MWAJIRI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MUDA WA MAOMBI: 28/06/2024 14/07/2024

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
  • Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  • Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi
  • Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake
  • Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

MSHAHARA NA POSHO
Malipo ya mshahara yatazingatia Mwongozo wa Afya wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline). Aidha posho nyingine zitalipwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

✅Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II – (NAFASI 08)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MASHARTI YA AJIRA: Kujitolea, Mkataba wa Mwaka 1

SIFA
Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

KAZI: Afisa Muuguzi Msaidizi
MWAJIRI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MUDA WA MAOMBI: 28/06/2024 14/07/2024

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kutoa huduma za uuguzi
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

MSHAHARA NA POSHO
Malipo ya mshahara yatazingatia Mwongozo wa Afya wa Taifa wa kujitolea wa Julai, 2021 (National Health Workers Volunteering Guideline). Aidha posho nyingine zitalipwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

✅Mteknolojia Vifaa Tiba Daraja la II – (NAFASI 01)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MASHARTI YA AJIRA: Kujitolea, Mkataba wa Mwaka 1

SIFA
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha nne na cheti cha ufundi cha mteknolojia Vifaa Tiba ngazi ya Stashahada (Diploma) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI: Mteknolojia Vifaa Tiba Daraja la ll
MWAJIRI: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini
MUDA WA MAOMBI: 28/06/2024 – 14/07/2024

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya kazi zote za fani ya vifaa tiba
  • Kufanya kazi ya kutengeneza vifaa tiba
  • Kuandaa mahitaji ya vifaa tiba vya hospitali
  • Na majukumu mengine utakayopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

Kuona Nafasi zote 54 za Kazi Kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini June 28-2024 tafadhali Donwload PDF hapa chini;

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

  • Waombaji wote wawe raia wa Tanzania wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wawasilishe barua ya maombi na nakala zifuatazo: –
  • Wasifu binafsi (CV).
  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
  • Vyeti vya Elimu ya Sekondari/ Msingi
  • Vyeti vya Utaalam katika fani husika.
  • Usajili (Full Registration) na Leseni hai kwa kada husika.
  • Muombaji aambatanishe picha ndogo (Passport size) mbili (2) kwenye barua ya maombi
  • Vyeti vilivyotolewa na Bodi ya mitihani za nje ya Tanzania vya elimu ya kidato cha nne (CSE) au elimu ya kidato cha sita (ACSE) vinapaswa kuthibitishwa na Baraza la Mitihani (NECTA).

JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi yawasilishwe kufikia au kabla ya tarehe 14.07.2024 saa tisa na nusu alasiri (1530HRS, kwa njia moja kati ya zifuatazo: –
Mtandao kwa barua pepe [email protected]
Kwa mkono ifike katika Ofisi ya Masjala ya Wazi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (Hakikisha unasaini katika kitabu baada kukabidhi).
Kwa Posta kupitia Anuani ifuatayo: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, S.L.P. 272,
MTWARA.

Tags:

Comments are closed.