NAFASI 958 za Afisa Kilimo Msaidizi MDAs na LGAs August 2024
NAFASI 958 za Afisa Kilimo Msaidizi MDAs na LGAs August 2024
NAFASI 958 za Afisa Kilimo Msaidizi MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 958 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.
✅AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (NAFASI 481)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio;
- Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio;
- Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora;
- Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti;
- Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi yambolea na madawa, pembejeo za kilimo;
- Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi,robo na mwaka ngazi ya Halmashauri;
- Kukusanya takwimu za mvua;
- Kushiriki katika “survey” za kilimo;
- Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
kutumia; - Kupanga mipango ya uzalishaji;
- Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi;
- Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo;
- Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima;
- Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu;
- Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;
- Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimoKuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji;
- Kutoa ushauri wa kilimo mseto;.
- Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira naKutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au Sita (VI) wenye stashahada
(Diploma)ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C.
✅AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III – (NAFASI 477
MAJUKUMU YA KAZI
- Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa;
- Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara;
- Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana zakilimo;
- Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika Kijiji;
- Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao;
- Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao;
- Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kilasiku;
- Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo (Opportunitiesand Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan (VADP); na
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada ya Kilimo kutoka
Vyuo vinavyotambuliwa naSerikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama
ifuatavyo;.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
Cheti cha kuzaliwa - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
Tags: 958 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024., MDAs & LGAs August 2024, MDAs & LGAs Jobs, NAFASI 958 za Afisa Kilimo Msaidizi MDAs na LGAs August 2024