RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024

Filed in Ajira, Michezo, TAMISEMI by on 06/04/2024

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024, The Ministry of Health Tanzania Vacancies Announcement, Ajira Mpya 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024, Nafasi 8900 za Kazi Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024, Ajira za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024.

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inatekeleza Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii nchini.

Kupitia Mpango huu, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapata Wahudumu wenye sifa zilizowekwa, kutoa mafunzo na kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika utekelezaji wa afya Jumuishi za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii ambapo Mpango unahitaji Wahudumu wawili (2) yaani Mwanaume na Mwanamke kwa kila Kitongoji/Mtaa.

“Mikakati hii ambayo tumeanza nayo ya utoaji wa elimu ya Lishe pamoja na Uzazi wa Mpango kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ili watumike kutoa elimu ya Afya hizo kwa wananchi kwa kuwa wao ndio wapo karibu zaidi na wananchi.” Amesema Waziri Ummy

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha hayo leo (Jana) Aprili 5, 2024 kwenye kikao kifupi baina ya Mawaziri kutoka Wizara za Kisekta na ugeni kutoka nchini Uingereza ukiongozwa na Waziri wa Uingereza wa Maendeleo na Afya Mhe. Andrew Mitchel.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Adolf Mkenda, Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. David Concar pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe

Katika kutekeleza Mpango huu, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI inawatangazia Wananchi kuwa Mpango huu kwa awamu ya kwanza utaanza katika Mikoa 10 na Halmashauri mbili (2) kwa kila Mkoa kama inavyoonekana katika Jedwali

Aidha, Utekelezaji wa Mpango huu utaendelea kwa awamu katika Mikoa na
Halmashauri zote za Tanzania Bara.

Wananchi wenye sifa stahiki ndani ya Mikoa 10 iliyooneshwa katika Jedwali hapo awali, wanahimizwa kuomba nafasi za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mitaa/Vitongoji vyote ndani ya Halmashauri zao.

Maombi yote yawasilishwe kwa Wakurugenzi waHalmashauri, ambao watasimamia zoezi la kuwachagua Wahudumu wenye sifa miongoni mwa waliotuma maombi kwa kuzingatia Miongozo iliyotolewa.

SIFA ZA WAOMBAJI:

  • Awe na utambulisho rasmi kama vile Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Mpiga Kura;
  • Awe amemaliza Elimu ya Sekondari (angalau Kidato cha Nne) na awe na
    Cheti cha Kuhitimu (Leaving Certificate);
  • Awe ni mkazi na kwa sasa anaishi Kitongoji/Kijiji na Mtaa husika;
  • Awe anafahamu lugha, utamaduni, mila na desturi za Jamii husika;
  • Akubalike Kimaadili na Kiutamaduni na jamii husika
  • Asiwe na historia ya vitendo vya uhalifu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto;
  • Awe na moyo wa kujituma, mchapakazi na mwenye ari ya kutumikia jamii;
  • Awe mwaminifu na mwenye uwezo wa kuweka taarifa za mteja kuwa siri;
  • Awe na utayari na uwezo wa kufanya kazi katika Kitongoji au Mtaa husika na;
  • Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 55.

Maombi yawasilishwe Ofisi ya Mtendaji wa Kata yakiambatanishwa na:

  • Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na kuwekwa saini ya mwombaji
  • Nakala ya Cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne (Form IV Leaving Certificate);
  • Picha mbili (2) za Passport Size;
  • Maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/namba ya simu ya kiganjani ya Wadhamini wasiopungua wawili (2).
  • Barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa wa eneo analotoka.

Mwisho wa kuwasilisha maombi haya ni wiki mbili (2) tangu tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili.

Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia Ofisi za Watendaji wa Kata
husika.

Imetolewa na:
KATIBU MKUU
S.L.P 743 DODOMA
06/04/2024

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024 DONWLOAD PDF

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii April 2024

Tags: , , , ,

Comments (3)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Gilliard Mmari says:

    Habari ya Leo naomba ikitokea tangazo kingine la ajira naomba nijukishwe kupitia email yangu
    Asante

  2. Ester ndile says:

    Ajira katika secta ya Afya