RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Nzega August 2024

Filed in Ajira by on 01/08/2024

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Nzega August 2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nzega August 2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nzega August 2024

NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Nzega August 2024,Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Nzega
anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi
zifuatazo :-

✅MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI (12)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji;
  • Katibu wa Kamati ya kijiji;
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na
    Halmashauri katika Kijiji;
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji;
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria
    nyingine zinazotumika katika Kijiji;
  • Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umasikini katika Kijiji;
  • Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umasikini katika Kijiji;
  • Kusimamia Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza
    kumbukumbu za walipa kodi; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI), awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa
au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI (03)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming
    Correspondence Register)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing
    CorrespondenceRegister)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji
  • Kurudisha majalada
    kwenye shubaka/kabati la
    majalada (Racks/FillingCabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo
ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa
kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (3)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
  • Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
    majukumu ya kazi
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
    Idara/ Kitengo/ sehemu husika
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi
  • Kufanya kazi nyingine atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI),
wenye stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha (NTA Level 6) ya
uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile; Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail
na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya
    Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na
    Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
    kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi
    ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates,
    – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, –
    Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
  • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa
    hatua za kisheria.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo
ielekezwe kwa

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega,
S.L.P 4,
NZEGA-TABORA

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa
kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags: ,

Comments are closed.