NAFASI za Madereva Nzega District Council August 07-2024
NAFASI za Madereva Nzega District Council August 07-2024
NAFASI za Madereva Nzega District Council August 07-2024, Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024
chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Nzega anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
- Kufanya usafi wa Gari;
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 nanusiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip)
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards)
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET)
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega,
S.L.P 4,
NZEGA-TABORA
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani
hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKILIWA
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
POST: DEREVA DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, More Details |
2024-08-22 Login to Apply |
Tags: NAFASI za Madereva Nzega District Council August 07-2024