NAFASI za 9 za Kazi Wilaya ya Mkuranga July 16-2024
NAFASI za 9 za Kazi Wilaya ya Mkuranga July 16-2024
NAFASI za 9 za Kazi Wilaya ya Mkuranga July 16-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Mkuranga amepokea Kibali cha Ajira mpya
kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA 16-07-2024
Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada Tisa (09) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-
✅MWANDISHI WENDESHA OFISI DARAJA LA II (“Office Management Secretary II”) NASAFI 05
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwalekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kati zingine. - Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu
ya kazi. - Kupokea majadala na kusambaza kwa Maofisa walio katika
Idara/Kitengo/sehemu husika, - Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne au sita wenye Stashahada (Diploma) ya
Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.Aidha wawe wamefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneo 100 kwa dakika moja na kupata
Programu za Kompyuta za Ofisi kama vile: Micro Soft Word, Powerpoit, Internet, Email na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali – TGS C
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 04
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua garia kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kufanya kazi ya kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na
- Kufanya Usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atavyoelekezwa na Msimamizi wake
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya Kidato cha Nne na kupata cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (01) bila kusababisha ajali.
Awe amehudhuria Mafunzo ya Msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au chuo Kingine kinachotambulisha na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzaniawenye Umri wa Miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuanisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa ZSekretarieti ya Ajira kwatika Utumishi wa
Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba za Simu zinazopatikana na Anwani ya
Barua pepe (email address) Pamoja na majina ya wadhamini (Referees)watatu wa kuaminika. - Provisional /’’Testimonials’’/’’Statement of Results’’na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form Iv na Form VI results) Havitakubaliwa.
- Waombaji wote waambanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Wanasheria/Wakili. - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, Wapitishe barua zao kwa maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na waajiri wa wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji kazi ambao teyari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliokom kalioko katika Utumishi na Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,2010
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Certificates, – Cheti cha Mtihani wa Kidati IV na Vi, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective
Boards) - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Uwasilishaji wa Taarifa za Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
- Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni 28 Julai, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa Pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA,
S.L.P 10
MKURANGA
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektoniki wa ajira (Recuritment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretatieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga More Details |
2024-07-28 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga More Details |
2024-07-28 Login to Apply |