RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Awali Na Msingi 2024/2025

Filed in Ajira by on 25/07/2024

NAFASI za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Awali Na Msingi 2024/2025

NAFASI za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Awali Na Msingi 2024/2025

NAFASI za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Awali Na Msingi 2024/2025

NAFASI za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Awali Na Msingi 2024/2025,Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi.

Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi na hisabati.

Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).

Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi na hisabati ni wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la kwanza hadi la tatu (I-III).

Mafunzo haya yatatolewa katika vyuo vya Serikali na Vyuo visivyo vya Serikali.

Vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali vitatoa mafunzo haya baada ya kuwasilisha maombi na kupata kibali cha Kamishna wa Elimu.

Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka
02) ni:

  • Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo
    ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
  • Walimu waliohitimu mafunzo ya Ualimu ngazi yabAstashahada (Cheti) ya
    Ualimu Elimu ya Awali au Msingi. Aidha waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu.

Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka
03) ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni:

Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science.

AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu (kozi) na vyuo vinavyotoa mafunzo husika.

STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI (MIAKA 02)

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

  • Wahitimu wa kidato cha nne, kidato cha sita na walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobaizinishwa katika tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi;
  • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa
    udahili wa Wizara ya Elimu,
    Sayansi na Teknolojia
    (https://tcm.moe.go.tz:8081);
  • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo
    husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki;
  • Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
  • Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu
    Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
  • Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia
    tarehe 25/08/2024) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa;
  • Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake.
  • Waombaji wote
    wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi; na
  • Majibu na fomu za kujiunga na Chuo kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali yatatolewa na vyuo husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20/08/2024.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags:

Comments are closed.