NAFASI za Watendaji na Madereva Wilaya ya Msalala June 28-2024
NAFASI za Watendaji na Madereva Wilaya ya Msalala June 28-2024
NAFASI za Watendaji na Madereva Wilaya ya Msalala June 28-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leo June 28-2024,Nafasi za Kazi za Madereva kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leo June 28-2024.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA 28-06-2024
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ni moja kati ya Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga iliyoanzishwa rasmi tarehe 01.07.2013, baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) Na 363.
Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya yapo katika kijiji cha Buganzo Kilichopo katika kata ya Ntobo, sehemu kubwa ya
shughuli za kiuchumi ni Kilimo, uchimbaji madini pamoja na biashara ndogondogo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Msalala anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa, kuomba kujaza nafasi za kazi katika kada zifuatazo.
✅DEREVA II – NAFASI (1),
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni daraja ‘C’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda
usiopungua miaka mitatu (3) bila kusababisha ajali, - Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
- Muombaji mwenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II atafikiriwa kwanza
Ngazi ya Mshahara: TGS B. Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
✅MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI TATU (3)
SIFA ZA MUOMBAJI,
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii,
Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali
Ngazi ya Mshahara: TGS. B, kwa kuzingatia viwango vya Serikali
MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia Ulinzi na Utawala Bora kwa Raia na mali zao. Kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Kijiji
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini
na kuongeza uzalishaji mali. - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbuu zote na nyaraka za Kijiji
- Kuwa mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
- Kupokea,kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na usiopungua umri wa miaka 18.
- Waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed
C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminik - Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma, na vyeti vya kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye ajira portal.
- Testimonials, “Provision Results”, “Statements of Results”, hati ya
matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA - Waombaji wote waweke picha mbili “Pasport Size” ya hivi karibuni katika ukrasa wa ajira portal
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11/07/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya Msalala
S.L.P 16
KAHAMA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa
kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Msalala More Details |
2024-07-12 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Msalala More Details |
2024-07-12 Login to Apply |
Tags: Nafasi za Kazi za Madereva kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leo June 28-2024., Nafasi za Kazi za Watendaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Leo June 28-2024, NAFASI za Watendaji na Madereva Wilaya ya Msalala June 28-2024