NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Kongwa June 11-2024
NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Kongwa June 11-2024
NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Kongwa June 11-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Leo June 11-2024, Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Leo tarehe 11-2024.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KONGWA 11-06-2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa ya kujaza nafasi Moja (01) ya Ajira ya Kudumu katika Kada ya Mtendaji wa Kijiji.
Daraja la III. Nafasi hii inatokana na Kibali Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA.228/613/01/a/090 ya tarehe 15 Machi, 2024.
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (1)
SIFA ZA MWOMBAJI:
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato Nne/Sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA Level 5) katika mojawapo ya Fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa
Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka ka tika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI:
- Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji .
- Kusimamia ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao. Kuwa Mlinzi wa Amani na msimamizi wa
Utawala bora katika Mtaa. - Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji.
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
- Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
- Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi.
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS B1
MASHARTI YA JUMLA:
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye Umri kati ya Miaka 18 hadi 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea Ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajiliya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae
(CV) yenye Anuani inayotumika, Namba za Simu na Anuani ya barua pepe (E-mail addres) pamoja na majina ya Wadhamini (Referees) watattu wa kuaminika. - ‘’Provisional/Testimonials/Statement of results’’ na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita) Form IV na VI results Slip) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji wote waambatishe Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Maombi yote yaambatane na Vyeti vya Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni Vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishiwa na Mamlaka (TCU NACTE na NECTA)
- Uwasilishaji wa Taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
- Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kingereza.
- Mwombaji awasilishe Picha moja ya hivi karibuni (Passport Size).
Muhimu: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwapamoja na Vyeti ya Elimu,
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Alhamis, tarehe 24 JUNI, 2024.
Aidha, Anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KONGWA,
S.L.P 57,
KONGWA – DODOMA.
Maombi yote ya kazi yatumwe Mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia Anuani ifuatayo; htts//:portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sekretatieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa (Recuitment Portal)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa More Details |
2024-06-24 Login to Apply |
Tags: Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Leo tarehe 11-2024., Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Leo June 11-2024, NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Kongwa June 11-2024