RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Mtwara 24-06-2024

Filed in Ajira by on 26/06/2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Mtwara 24-06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Mtwara 24-06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara June 24-2024, Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Leo Juni 24-2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Mtwara 24-06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya Ya Mtwara 24-06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara June 24-2024, Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Leo Juni 24-2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MTWARA 26-06-2024

Halmashauri ya Wilaya Mtwara inatangaza nafasi za kazi kwa wananchi wenye sifa za kuwa Watendaji wa Vijiji kufuatia kupata kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb.Na. FA.228/613/01/B/094 cha tarehe 22/04/2024 kama ifuatavyo;

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 2.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III;

  • Kuwa Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa rai ana mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji
  • Kuwa katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
    kuongeza uzalishaji mali
  • Kuwa kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
  • Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne au cha sita na mafunzo ya Astashahada
/ cheti katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii katika chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Watumishi wa Serikali, mshahara utakuwa ni TGS B.1.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza
    (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
    (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa
    za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,
    – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from
    Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 July, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mtwara,
S.L.P. 528,
MTWARA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF

Tags: , ,

Comments are closed.