RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024 

Filed in Ajira, Michezo by on 19/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024 

NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024,Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Wilaya ya Kibondo Kigoma June 19-2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma June 19-2024.

NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024

NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024,Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Wilaya ya Kibondo Kigoma June 19-2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma June 19-2024.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na mchakato wa maandalizi ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Hii ni kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Namba 2 ya Mwaka 2024 kanuni ya 12 kifungu kidogo cha 1(b-f).

Hivyo basi, Afisa Mwadikishaji wa Jimbo la Muhambwe anawatangazia waombaji wote waliochaguliwa kwa nafasi ya Waandikishaji na Waendeshaji wa vifaa vya bayometriki kwaajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kufika kwenye usaili siku ya Jumamosi tarehe 22/6/2024 kuanzia saa 2.30 asubuhi katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya Kibondo.

Wasailiwa wanatakiwa kufika wakiwa na vyeti vyao halisi walivyovitumia wakati wa kuomba nafasi hizo na kitambulisho cha Taifa/Mpiga kura.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi haitahusika na gharama zozote atakazotumia mwombaji wakati wa usaili.

ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI KWA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI KWA AJILI YA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO DOWNLOAD PDF

NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Kibondo June 19-2024

WOTE WENYE SIFA ZA KUANDIKISHWA KUWA WAPIGA KURA WATAANDIKISHWA HATA KAMA HAWANA KITAMBULISHO CHA NIDA

WOTE WENYE SIFA ZA KUANDIKISHWA KUWA WAPIGA KURA WATAANDIKISHWA HATA KAMA HAWANA KITAMBULISHO CHA NIDA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema watu wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wataandikishwa hata kama hawana kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile tarehe 15 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri.

Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024. Baadae Tume itafanya mikutano na wadau kwenye mikoa yote kwa kuzingatia ratiba ya uboreshaji wa Daftari.

Mikutano hiyo ina lengo Ia kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.

“Kuwa na kadi ya NIDA sio kigezo cha kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu Ia Wapiga Kura. Wananchi wote wenye sifa wataandikishwa bila kujali kama wana kadi ya NIDA au la,” amesema Bi. Aswile.

Ameyataja mambo yatakayohusika kwenye uboreshaji wa daftari kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.

Mambo mengine ni kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.