NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Urambo July 2024
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Urambo July 2024
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Urambo July 2024, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora July 07-2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Urambo Tabora , Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Urambo July 06-2024.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIMBO LA URAMBO
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Urambo, anawaalika kuhudhuria Usaili wa Kazi ya Mwandishi Msaidizi na Mwendesha Mshine (BVR OPERATORS) ngazi ya Vituo.
Usaili utafanyika tarehe 11/07/2024 kwa kituo cha ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo na 12/07/2024 kwa kituo cha Usongelani shule ya Sekondari iliyopo kata ya ussoke.
Aidha, muda wa kuanza Usaili kwa kila kituo ni saa 2:00 Asubuhi hivyo waombaji wazingatie muda.
Waombaji watajigharamia Nauli na Chakula.
Orodha ya majina walioitwa kwenye Usaili inapatikana kwenye PDF hapa chini;
WALWASAILIWA JIMBO LA URAMBO DONWLOAD PDF
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Urambo July 2024
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema watu wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wataandikishwa hata kama hawana kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile tarehe 15 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri.
Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024. Baadae Tume itafanya mikutano na wadau kwenye mikoa yote kwa kuzingatia ratiba ya uboreshaji wa Daftari.
Mikutano hiyo ina lengo Ia kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.
“Kuwa na kadi ya NIDA sio kigezo cha kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu Ia Wapiga Kura. Wananchi wote wenye sifa wataandikishwa bila kujali kama wana kadi ya NIDA au la,” amesema Bi. Aswile.
Ameyataja mambo yatakayohusika kwenye uboreshaji wa daftari kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.
Mambo mengine ni kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.
Tags: Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Urambo Tabora, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Urambo July 06-2024., Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora July 07-2024, NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Urambo July 2024